NA FREDY MGUNDA, IRINGA
Leo ni siku ya tatu kwa kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Ltd toka
imetenga pakiti 120,000 za maziwa yenye thamani ya Sh Milioni 60 zilizoanza
kugaiwa bure kwa wanafunzi zaidi ya 30,000 wa shule za msingi za serikali na
binafsi za mjini Iringa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yake ya wiki ya maziwa.
Kampeni ya kugawa maziwa hayo ilizinduliwa juzi katika
shule za manispaa ya Iringa huku Mratibu wa maziwa wa kampuni hiyo, Lipita
Mtimila akisema hatua hiyo ni muendelezo wa mikakati yao ya kudumu inayolenga kuhamasisha
jamii ya wana Iringa kuongeza kiwango cha unywaji maziwa kutoka chini ya
asilimia 10 za sasa hadi asilimia 40.
Alisema takwimu za sasa zinaonesha kiwango cha maziwa yanayouzwa
kwa siku katika mji huo kinakadiriwa kuwa lita 3,500 ambazo kati yake lita
1,500 ni zile zilizosindikwa na lita 2,000 zinazouzwa kwa walaji bila
kusindikwa.
“Tunawahimza wadau wote wa maziwa kushirikiana na kampuni yetu ya
maziwa ya Asas kuhamasisha unywaji wa maziwa, sio mjini Iringa pekee lakini pia
na maeneo mengine yote nchini,” alisema.
Wakiipongeza kampuni hiyo na kampeni yake ya unywaji maziwa mjini
Iringa baadhi ya walimu walisema maziwa ni chakula ambacho kama kitatumiwa kama
inavyoshauriwa mchango wake ni mkubwa katika kutokomeza magonjwa
yanayotokana na ukosefu wa lishe bora ukiwemo utapiamlo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mshikamano, Haiba Roy
alisema ipo haja ya kuanzisha kampeni ya unywaji wa maziwa mashuleni kila siku,
mpango utakaowasaidia kiafya wanafunzi wengi wakiwemo wale wanaokwenda shule
wakiwa hawajapata mlo wowote toka majumbani mwao.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mtwivilla, Frolian Kilumile
aliipongeza kampeni ya kampuni hiyo akisema inasaidia kuwakumbusha wazazi kuwa
na utamaduni wa kununua maziwa kwa kuzingatia mahitaji ya watoto.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hizo walisema wengi wao hawajawahi
kunywa maziwa wakiwa majumbani mwao na hawaelewi sababu za kukosa kinywaji
hicho chenye ladha nzuri na kinachoelezwa kuwa na faida nyingi kwa ukuaji wa
mwili na akili zao.
Mmoja wa wanafunzi hao, Thobias Mlanzi alisema amekunywa mara
kadhaa maziwa kupitia kampeni ya kampuni hiyo na anaona haja ya kuwashawishi
wazazi wake aliosema wana uwezo wa kumudu gharama kumtengea Sh 500 kila siku
kwa ajili ya maziwa hata kama wao hawana mapenzi na kinywaji hicho.
Akizungumzia mipango ya kusogeza zaidi huduma ya maziwa karibu na
mlaji, Mtimila alisema mbali na kupatikana katika maduka mbalimbali mjini
Iringa na maeneo mengi nchini, wako mbioni kutumia teknolojia mpya ya uuzaji wa
bidhaa hiyo kwa mfumo unaofanana na mashine za kutolea au kuweka fedha (ATM).
“Tutafunga mashine za kuuza maziwa zinazofanana na ATM, mteja
anayehitaji maziwa atatumbukiza fedha katika mashine hiyo ambayo itatoa maziwa
kulingana na thamani ya fedha aliyotumbikiza,” alisema.
Pamoja na mpango huo, mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Ahmed Salim Abri
alisema kampuni yao inaendelea na upanuzi wa kiwanda chao cha Iringa
utakaokwenda sambamba na matumizi ya teknolojia ya UHT kutengeneza aina
mbalimbali za maziwa.
"Teknolojia hii ya Ultra High Temperature inawezesha maziwa yanayosindikwa
kukaa kwa muda mrefu, hadi miezi sita bila kuharibika hata yakiwekwa katika
maeneo yasio na mashine za kuyapooza," alisem.
Alisema matumizi ya teknolojia hiyo yatakiwezesha kiwanda chao kuongeza
uzalishaji na kupanua soko lake hadi katika maeneo ambayo matumizi ya majokofu
ni madogo.
Pamoja na mpango huo, mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Ahmed Salim Abri alisema kampuni yao inaendelea na upanuzi wa kiwanda chao cha Iringa utakaokwenda sambamba na matumizi ya teknolojia ya UHT kutengeneza aina mbalimbali za maziwa.
"Teknolojia hii ya Ultra High Temperature inawezesha maziwa yanayosindikwa kukaa kwa muda mrefu, hadi miezi sita bila kuharibika hata yakiwekwa katika maeneo yasio na mashine za kuyapooza," alisem.
Alisema matumizi ya teknolojia hiyo yatakiwezesha kiwanda chao kuongeza uzalishaji na kupanua soko lake hadi katika maeneo ambayo matumizi ya majokofu ni madogo.
0 comments:
Post a Comment