Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania tarehe 25 Mei, 2018, lilipitisha Makadirio ya Jumla ya Shilingi 1,692,286,014,000 kwa ajili ya matumizi
ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2018/19.
Baada ya kupitishwa
kwa Bajeti hiyo, katika kikao na Watendaji wa Wizara na Taasisi, Waziri wa
Nishati Dkt. Medard Kalemani alitoa
pongezi za pekee kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu kwa namna ambavyo
amekuwa akisimamia utekelezaji wa
majukumu ya Sekta na kueleza kuwa ndani ya kipindi kifupi alichokaa wizarani
tangu kuteuliwa kwake, Naibu Waziri amefanya kazi kubwa.
Pia, alipongeza Watendaji
na Watumishi wa Wizara na Taasisi zake kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha
wakati wote wa utekelezaji wa Majukumu ya Wizara.
Alieleza kuwa,
pongezi zilizotolewa kwa Wizara na
Wabunge wakati wa kuwasilisha Bajeti ni pongezi za Wizara nzima na hivyo
kuwataka watumishi wote wa wizara
kuzilinda pongezi hizo, kujipima na kujitafakari na kutekeleza yote yaliyoshauriwa
na Wabunge hao.
Aliwataka watumishi
wote wa wizara ya Nishati kuwasilikiza wananchi kwa kuwa kufanya hivyo kunatoa
nafasi ya kuchuja mambo na kuyafanyia kazi kikamilifu.
Pia, aliwataka
watumishi wote wa Wizara na Taasisi kulala na masuala ya muhimu vichwani mwao kwa
ajili ya kuendeleza sekta.
Kwa upande wake,
Naibu Waziri Subira Mgalu alipongeza ushirikiano uliooneshwa na watumishi wa
Wizara na Nishati na taasisi zake na hivyo kuwataka kujipanga kwa ajili ya
utekelezaji wa majukumu ya Bajeti ya
Mwaka wa Fedha 2018/19.
Naye, Katibu Mkuu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Dkt. Hamisi
Mwinyimvua, alisifu ushirikiano uliopo katika Wizara na Taasisi zake na hivyo
kuwataka watumishi wote kuendelea na ari hiyo.
0 comments:
Post a Comment