Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia)
akikabidhiwa Rasimu ya mwisho ya
Sera ya Taifa ya Misitu na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula
na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred Kafeero (katikati) katika
hafla ya makabidhiano iliyofanyika
leo katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na
Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia)
akizungumza mara baada ya makabidhiano ya
Rasimu ya mwisho ya Sera ya
Taifa ya Misitu katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo katika makao makuu ya
ya Wizara mjini Dodoma.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred Kafeero (wa
kwanza kushoto) akizungumza mara baada ya makabidhiano
ya nakala ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu katika hafla ya
makabidhiano iliyofanyika katika
makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa ( wa pili kushoto) akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred Kafeero (wa pili kulia) kabla ya makabidhiano ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma
..............................................
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imekabidhiwa rasimu
ya mwisho ya sera ya Taifa ya Misitu na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja
wa Mataifa (FAO) kufuatia kukamilika kwa
mchakato uliowashirikisha wadau wote muhimu.
Hatua hiyo inafuatia ikiwa ni mwaka mmoja sasa ambapo FAO na
wizara ya Maliasili na Utalii ziliposainiana mkataba wa msaada wa Kitaalamu
kuisaidia serikali kukamilisha Mapitio ya Sera ya Taifa ya Misitu ambayo ilipitishwa mwaka 1998.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence
Milanzi amesema Tanzania inakabiliwa changamoto katika
kuthibiti rasilimali misitu kwa kuwa sera ya misitu inayotumika kwa sasa ni ya
zamani hali inayochangia kushindwa kuendana na kasi ya maendeleo sasa.
Ameyasema hayo leo tarehe
10 April, 2018 katika hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika
makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma baina yake, na Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred
Kafeero.
Milanzi amesema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka wakati
ambapo nchi inakabiliwa na changamoto nyingi za uharaibifu wa misitu.
‘’Tunahitaji sera dhabiti ya kukabiliana na masuala mbalimbali yanayohusu
uharibifu wa rasilimali za misitu’’ alisisitiza Milanzi.
Kwa upande wake, Kafeero alisema alisema FAO imepiga hatua kubwa
za mafanikio katika kukamilisha mchakato
wa kuandaa rasmu hiyo ambayo ni shirikishi.
‘’Tayari FAO imesaidia nchi nyingi kwenye maeneo hayo lengo likiwa
kuhakikisha kuwa sera hiyo inatilia maanani masuala ya maendeleleo ya kitaifa
na kimataifa.
Aidha, Kafeero alisema misitu ni moja ya maeneo ya majukumu makuu
ya FAO kwa kuwa ni moja ya maeneo muhimu yanayohusiana na matumizi endelevu ya
maliasili, uhakika wa chakula na lishe pamoja na maendeleo ya uchumi kwa
ujumla.
Wakati huo huo, FAO pamoja na Serikali wanamalizia taratibu za
kuandaa mkakati wa kuitekeleza Sera hiyo
ili iweze kuleta matokeo chanya
yaliyokusudiwa katika misitu nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence
Milanzi ( wa kwanza kulia) akikabidhiwa nakala
ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya
Taifa ya Misitu na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa
Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred Kafeero (wa pili kushoto) katika hafla ya
makabidhiano iliyofanyika katika makao
makuu ya ya Wizara mjini Dodoma. Wa kwnza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Misitu na Nyuki.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence
Milanzi ( wa kwanza kulia) akizungumza mara baada ya makabidhiano ya nakala
ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya
Taifa ya Misitu katika hafla ya makabidhiano
iliyofanyika katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma. Wa kwanza
kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa
Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred Kafeero (wa pili kushoto) akizungumza mara baada ya makabidhiano ya nakala
ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya
Taifa ya Misitu katika hafla ya makabidhiano
iliyofanyika katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma. Wa kwanza
kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel
Mwakalukwa akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,
Maj. Gen Gaudence Milanzi na Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) hapa nchini,
Fred Kafeero (wa pili kushoto) kabla ya
makabidhiano ya Rasimu ya mwisho ya Sera
ya Taifa ya Misitu katika hafla ya makabidhiano
iliyofanyika katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma.
Baadhi ya nakala ya Rasimu
ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu
iliyokabidhiwa leo na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Kimataifa (FAO)
kwa serikali ya Tanzania katika hafla
iliyofanyika leo katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment