Baadhi ya pamba zikiwa shambani kabla ya kuvunwa. |
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Charles Kabeho,akiweka jiwe la msingi kwenye shamba la pamba kwenye kijiji cha Nyamalimbe. |
Watoto ambao ni yatima wakipewa zawadi na Kiongozi wa mbio za mwenge Charles Kabeho kwenye Kijiji cha Bujura wilayani Geita. |
Na Joel Maduka-Geita
Serikali imewahakikishia
mazingira yaliyo salama wakulima wa zao la pamba ikiwa ni pamoja na kununuliwa
kwa zao hilo bila ya kukopwa kwa msimu
wa pamba ambao unatarajia kuanza tarehe 1 Mei mwaka huu .
Hayo
yameelezwa na kiongozi wa mbio za mwenge
wa uhuru , Charles Kabeho wakati
akifungua mradi wa zao la pamba katika kijiji cha Nyamalimbe Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo alisema serikali imejipanga kuhakikisha mkulima wa
pamba mwaka huu ananufaika na zao hilo.
“ Zao la
Pamba linamanufaa kwa mkulima na serikali kwani zao ambalo linatengeneza nguo kuliko kusubili kuletewa
mitumba kutoka nje hivyo tulithamini zao hili kwani linasaidia pia kuondoa
umaskini katika familia”Alisisitiza Kabeho.
Mussa Kabehe
ambaye ni Mkulima wa zao hilo alisema kwa sasa kutokana na hali ya hewa na mvua
kunyesha kwa wingi wamekuwa na matumaini machache ya kupata pamba Nyingi kwani
asilimia kuwa zimeharibikia shambani na kwamba awana matarajio ya kuzalisha
pamba Nyingi zaidi ingawa kwa mwaka huu wengi walijitokeza kulima pamba.
Kiongozi
huyo wa mwenge pia amefungua miradi 12 katika
Halmashauli ya Wilaya ya Geita iliyo gharimu kiasi cha shilingi bilioni tano na milioni
miatatu ambapo pia kiongozi huyo aliwakumbusha wananchi wa kijiji hicho
kutojihusisha na suara la rushwa kwa ni adui
wa haki.
0 comments:
Post a Comment