Mhe. Charles J. Mwijage (Mb), Waziri wa viwanda, biashara
na uwekezaji, akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika
halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018. Picha Zote Na Mathias Canal, NFRA
Baadhi ya wakuu wa mikoa inoyozalisha Pamba kwa wingi wakifatilia mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Mgeni-Rasmi Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, Mhe. Charles J. Mwijage (Mb), akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Naibu waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt Mary Mwanjelwa akijadiliana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Antony Mtaka wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Waziri wa kilimo, Mhe. Dkt Charles Tizebawakati akifatilia kwa makini mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Baadhi ya wadau wa sekta ya pamba wakifatilia kwa makini mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Na Mathias Canal,
Dodoma
Serikali
kwa kushirikiana na viwanda vya nguo na mavazi imeanzisha mpango maalum wa
kutoa mafunzo ya ushonaji kwa vijana kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya viwanda
vya nguo.
Upatikanaji
wa ujuzi wa aina hiyo utapunguza gharama kwa wawekezaji na kuongeza ufanisi
katika uzalishaji. Vilevile, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
kupitia msaada wa Gatsby Africa, kimeendelea kutoa mafunzo ya Shahada ya
Teknolojia ya Nguo (Textile Degree) ambapo, mwaka 2016/2017, Chuo kilitoa
wahitimu 44 ikilinganishwa na wahitimu 13 kwa mwaka 2015/2016. Lengo ni
kuhakikisha kuwa kuna wataalam wa kutosha wa fani ya ubunifu na uzalishaji
mavazi nchini.
Hayo yamebainishwa na Mhe. Charles J. Mwijage (Mb),
Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, wakati akifungua mkutano wa wadau wa
sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini
Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Alisema kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazozalisha pamba kwa kiasi kikubwa barani
Afrika, ikiwa na zaidi ya wakulima 500,000 wanaolima pamba katika eneo
linalokadiriwa kufikia hekta 412,000 katika mikoa 13 nchini. Sekta ya nguo na mavazi ni moja ya sekta za Kipaumbele katika kusukuma
gurudumu la maendeleo nchini na inahusisha mnyororo mrefu wa uongezaji thamani
kuanzia kuchambua pamba (ginneries); kusokota nyuzi (spinning); kuseketa
vitambaa (weaving); kufuma vitambaa (knitting), kuchapa na kutia rangi (processing) na kushona mavazi (garments).
Aliongezaa kuwa
Sekta hii ni moja ya sekta muhimu katika
kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuanzisha viwanda vinavyoajiri watu wengi kwa
wakati mmoja. Sekta hii itawezesha kupunguza uingizaji wa nguo kutoka nje na
kuongeza matumizi ya pamba inayolimwa nchini pamoja na malighafi nyingine
zinazopatikana nchini kama vile magadi na gesi asilia.
Hata hivyo, Serikali imeendelea kuzishawishi taasisi za Umma kwa kuanzia
majeshi na hospitali ili wanunue nguo na mavazi yanayozalishwa na viwanda vya
ndani. Lengo ni kuhakikisha kuwa
utaratibu wa makusudi unawekwa kwa Taasisi za umma kutumia bidhaa
zinazozalishwa na viwanda vyetu hapa nchini. Kwa mfano uvaaji wa fulana aina ya
Polo Shirt kwa wafanyakazi wote katika siku moja ya wiki, na pia wanafunzi wote
shule za msingi na sekondari kuvaa sare hizo. Inakadiriwa kuwa kuna jumla ya
wanafunzi milioni 15 na wafanyakazi wa sekta zote za umma wanafika 25,000.
Mhe
Mwijage alisema kuwa Utengenezaji
wa fulana moja ya polo unakadiriwa kutumia wastani wa gramu 300 za pamba, sketi
moja inakadiriwa kutumia gramu 600 za pamba, kaptula moja inakadiriwa kutumia
gramu 600 za pamba. Hivyo jumla ya gramu 900 za pamba zitahitajika kutengeneza
sare kwa mwanafunzi mmoja awe wa kike au wa kiume.
Kama ikikadiriwa kila mwanafunzi atavaa wastani wa
sare (sketi & shati au kaptula na shati) mbili tu kwa mwaka gramu 1800
(sawa na kilo 1.8) za pamba zitahitajika kwa mwanafunzi mmoja, hivyo wastani wa
kilo 27,000,000 (sawa na tani 27,000) zitahitajika kwa mwaka. Endapo mahitaji
yaliyokusudiwa yakipitishwa tunategemea kwamba viwanda vya ndani vitakuwa na
uwezo wa kutumia asilimia 17 ya pamba yote inayozalishwa nchini kwa mwaka. Hii
itahamasisha uzalishaji wa pamba, kuongeza ajira na kuongeza kipato.
“Serikali inakamilisha taratibu za kuidhinisha
‘’ Blue Print’’ ambayo imeainisha maeneo ya kufanyia
maboresho ya Kisera na Kisheria ili kuhamasisha uwekezaji katika Sekta
mbalimbali za uchumi ikiwemo sekta ya pamba nguo na mavazi” Alikaririwa Mhe Mwijage
Pia,aliwashukuru
Wadau wa sekta ndogo ya pamba, nguo na Mavazi kwa kazi kubwa wanayofanya katika
uzalishaji, biashara na wadau wengine kwa michango yao katika kuendeleza sekta
hii.
Mkutano huo umehusisha Wizari ya Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara
wa Fedha na Mipango, Wizara ya Kilimo; Waheshimiwa Wenyeviti wa Kamati za
Kudumu za Bunge za Viwanda, Biashara na Mazingira; Bajeti; Kilimo, Mifugo na
Maji; na Uwekezaji Mitaji ya Umma, Wakuu wa Mikoa; Makatibu Wakuu, Wawakilishi
wa Sekta Binafsi, Maafisa wa Serikali na Taasisi za Serikali.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment