NA LUSUNGU
HELELA-SHINYANGA
Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak amewatahadhalisha wananchi kuwa yeyote
atakayeharibu misitu kwa kukata au kuingiza mifugo kwenye misitu atachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza
jana wilayani Kishapu wakati wa kongamano ambalo lilikuwa ni
sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani
humo, Mkuu wa
Mkoa alipiga marufuku kukata miti bila
ruhusa yake au ya Mkuu wa wilaya.
Telak alisema
marufu hiyo imekuja kwa kuchelewa kwa vile hatua iliyofikia katika Wilaya hiyo inatisha
hakuna mahindi yanayostawi kutokana
na kutokuwa na mvua ya kutosha.
‘’Mtu
yeyote atakayekata miti ajiandae kupelekwa jela
kwa vile kukata miti katika wilaya hii ni sawa na uuaji.’’ alisema Telak
Alifafanua
kuwa mtu yeyote atakayetaka kukata miti hata ule uliopo uwanjani pake ni lazima
aombe kibali kwa wahusika na atakayekiuka kukata bila kibali ajue jela
inamwita.
Wakati huo huo, Telak alitoa agizo kwa wakuu wa wilaya wote
kuhakikisha wanawakamata wale wote
watakaoingiza mifugo kwenye maeneo yaliyopandwa miti.
Aliongeza
kuwa uharibifu wa misitu unaoendelea
kufanyika katika maeneo hayo unazidi
kuathiri hata mifugo kutokana na kukosekana kwa malisho kwa vile
hakuna mvua inayonyesha.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Ezekiel Mwakalukwa alisema suala la kulinda misitu linahitaji
ushirikiano kutoka kwa jamii, wizara pekee haiwezi.
Alisema tatizo
la uharibifu wa misitu katika wilaya ya Kishapu limechochea Idara kutengeneza
kanzidata itakayosaidia kuzibana Halmashauri kujua imepanda miti mingapi na
kati ya hiyo mingapi imepona.
‘’Tunaanza mwaka huu kukagua ili kujua miti hiyo imepandwa wapi na
maendeleo yake yakoje’’ alisisitiza Mwakalukwa.
Amesema
hali hiyo itasaidia kuthibiti Halmashauri ambazo zimekuwa zikitaja idadi kubwa
ya miti iliyopandwa kila mwaka lakini miti hiyo imekuwa haionekani ikikua na
pale unapohitaji kupelekwa ukaone miti hiyo
visingizio lukuki vimekuwa vikiibuka.
Maadhimisho ya wiki ya
upandaji miti Kitaifa yanafanyika Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ambapo
kauli mbinu yake ni Tanzania ya kijani inawezekana panda miti kwa maendeleo ya
viwanda
0 comments:
Post a Comment