Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, leo tarehe 6 Aprili 2018, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mohamed Maje kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.
Taarifa ya utenguzi huo imetolewa leo na Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Mhandisi Alhaji Mussa Iyombe mjini Dodoma.
Utenguzi wa Mohamad Maje unafuatia taarifa iliyotolewa na Tume iliyoundwa kukagua utendaji wake wa kazi na kubaini kuwa ameshindwa kusimamia na kudhibiti mapato ya Halmashauri hivyo kupelekea upotevu wa fedha.
"Hadi kufikia robo tatu ya mwaka wa fedha, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imekusanya mapato kwa asilimia 24 tu pamoja na kuwa Halmashauri hiyo ni kongwe yenye vyanzo vingi vya mapato" alieleza katibu Mkuu Iyombe.
0 comments:
Post a Comment