Afisa Kilimo Wilayaya Kibiti Bwenda Ismail (kulia) akiwa na AfisaUgani wa wilaya hiyo Organess Semwenda wakiangalia muhogo unaolimwa katika shamba la Kibiti Farm Estate lilipo kata ya Bungu wilaya ya Kibiti.
Meneja wakiwanda cha kusindika muhogo cha Ukaya kilichopo Mkuranga Joseph Mtanga (kulia) akimueleza Afisa Mazao wa Wilaya hiyo Derick Samuel namna kiwanda chake kilivyokwama kuendelea nauzalishaji kutokana na kukosekana kwa umeme.
Baadhi ya wakulima wa zao la muhogo wilaya ya Mkuranga wakiwa katika picha ya pamoja.
Na
Munir Shemweta, Pwani
Mkoa
wa Pwani umeanza uhamasishaji wa uwekezaji katika zao la muhogo ili kuwawezesha
wakulima kujiongezea kipato sambamba na kuendanana soko la China ambapo
Tanzania imepata fursa kuuza muhogo nchini humo.
Hali
hiyo imebainika mwishoni mwa wiki wakati maofisa kutoka Wizara ya Kilimo walipotembelea
mkoa huo ikiwa ni mkakati wa wizara kuhamasisha ulimaji zao la muhogo na kuangalia
changamoto zake kwal engo la kuongeza tija na uzalishaji waza ohilo.
Akielezea
harakati za wilaya ya Kibiti katika kuhamasisha
zao la muhogo Afisa Kilimo wa Wilaya hiyo Bw. Bwenda Ismail alisema, uhamasishaji
huo unaenda sambamba na utoaji mafunzo, utoaji mbegu bora kwa wakulima pamoja na
kuhakikisha kila kaya inakuwa na hekari moja ya muhogo jambo litakaloongeza uzalishaji.
Kwa mujibu wa Ismail sasa hivi zao la muhogo katika wilaya ya kibiti limekuwa
la kibiashara na hali hiyo inatokana na usafirishwaji wa muhogo mbichi kwa wingi
kila siku kutoka wilaya hiyo kuenda dar es salaam.
Alisema
kuwa, hatua nyingine inayofanywa na halmashauri ya wilaya ya Kibiti ni kusaidia
wakulima katika uuzaji muhogo hasa baada
ya kubainika wakulima katika wilaya hiyo wamekuwa wakipunjwa wakati wakuuza muhogo
kwa wafanyabiashara na sasa wilaya imejenga soko la pamoja lililogharimu milioni
65 na mategemeo ya wilaya ni kuwa muhogo utauzwa kwa vipimo stahiki tofauti na sasa
ambapo wakulima wanapunjwa kwa mihogo kutenganishwa ile mikubwa na midogo.
Afisa
kilimo huyo wa wilaya ya Kibiti alisema, uhamasishaji umewekwa pia katika ujenzi
wa viwanda lengo likiwa kuhakikisha muhogo unaonunuliwa kutoka kwa wakulima unasindikwa
sambambana kuhakikisha wilaya kibiti m inatenga maeneo kwa ajili ya matumizi
bora ya ardhi, wawekezaji wakubwa, wakati na wadogo pamoja na maeneo kwa ajili ya
vijana na msisitizo ukiwa kila kata itenge eneo.
Kwa
sasa Wilaya ya Kibiti umekamilisha sheria ndogo ambapo kila kaya itatakiwa kulima
zao la muhogo jambo litakalosaidia kusukuma watu kuingia shambani ikiwemo vijana
ambapo sasa watalazimika kuingia katika kilimo ili kuendana na kasi ya Tanzania
ya viwanda na soko la china la muhogo kwa kuzalisha muhogo wa kutosha.
Kwa
upande wa wilaya ya Mkuranga, serikali wilayani humo katika bajeti yake imekuwa
ikitenga fedha kwa ajili ya kununua na kusambaza mbegu za muhogo kwa wakulima mbalimbali.
Afisa Kilimo wilayani humo Bi. Julita Bulali amebainisha kuwa kutokana na jitihada
za kusambaza mbegu kwa wakulima kumekuwa na mwitikio mkubwa wa watu kuwekeza katika
zao la muhogo.
Hata
hivyo, changamoto kubwa katika wilaya hiyo ni kusitishwa kwa huduma katika kiwanda
cha Ukaya farm ambacho imekuwa mkombozi mkubwa wa kununua muhogo kutoka kwa wakulima
kutokana na kukosekana kwa umeme katika kiwanda hicho.
Kwa
mujibu wa meneja wa kiwanda hicho bw. Joseph Mtanga, awali kiwanda hicho kilikuwa
kikitumia jenereta lakini mara baada ya kuharibika najitihada za kupataumeme kutoka
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kushindikana shughuli za kiwanda zimesimama
na hivyo kuwakosesha wakulima kuuza muhogo katika kiwanda hicho.
Meneja huyo wa
kiwanda cha Ukaya Farm alisema kiwanda chake hununua wastani wa tani nne mpaka mpaka
kumi na mbili kwa siku kutoka kwa wakulima na kusitishwa kwa usindikaji kumesababisha
pia ajira za watu thelathini mpaka arobaini kusimama.
Baadhi
ya wakulima mkoani humo walisema wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa
soko la uhakika jambo linalosababishwa mzunguko wa biashara kutoenda vizuri.
Walisema
biashara ya muhogo wakati mwingine inakwama kutokana na masuala ya kisera ambapo
bidhaa zao zinahitaji kuhalalishwana shirika la viwanga Tanzania (TBS) jambo linalofanya
kushindwa kuingia katika ushindani kutokana na kutokidhi vigezo. Pia
ukosekanaji wa vipimo stahiki katika uuzaji muhogo katika magari unawanyonya wakulima
kwa kuwa bei wanayakubaliana mazao yakiwa shambani tofauti nabei wanayouza.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment