Jana 14 Aprili 2018 timu ya Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), walianza upasuaji wa watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Zoezi gilo litafanyika Wilayani Nachingwea kwa siku tatu kuanzia Jana mpaka jumatatu 16 Aprili 2018, ambapo pia madaktari hao watafanya clinic kwa walioshindwa kufika MOI siku za nyuma.
Zoezi limefanikiwa ambapo watoto 15 watafanyiwa upasuaji, na wengine watapata ushauri wa Kitabibu.
Akizungumzia huduma hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango, alisema kuwa anajivunia kusababisha kupatikana kwa huduma hiyo muhimu kwa watoto wa Nachingwea Mkoa wa Lindi na mikoa ya jirani, hususani Mtwara na Ruvuma.
"Natoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa Uongozi wa MOI kwa kukubali ombi langu na kunipa ushirikiano tangu mwanzo wa kampeni hii hadi sasa tunavyohitimisha zoezi hili kwa kukamilisha matibabu. Mungu ataweka baraka zake" Alikaririwa Mhe Muwango
MWISHO
0 comments:
Post a Comment