Na Florah Raphael.
Mkuu wa wilaya ya kigamboni kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama leo wametembelea kata ya Pemba mnazi eneo la Yaleyale panu kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Alhamisi ya wiki iliyopita walipokuwa wakikagua majengo yaliyopo pembezoni mwa fukwe za bahari.
Akiongea na vyombo vya habari katika matembezi hayo Mh.Hashim Mgandilwa amesema kuwa takribani wiki mbili zilizopita walikuwa wanatembelea maeneo ya fukwe za bahari ili kufanya ukaguzi kutokana na wilaya hiyo ya kigamboni kuwa lango la biashara haramu na wahamiaji halamu.
Pia amesema kuwa katika ukaguzi huo waliofanya eneo linalomilikiwa na mwekezaji wa Lake oil lilikutwa na tatizo kwa kuwa na gati linaloweza kutumiwa na chombo chochote cha maji katika kushusha na kupakia mzigo wowote na kuagiza gati hilo kubomolewa ndani ya siku tano lakini maagizo hayo yamekiukwa ambapo utejelezaji umeanza kutekelezwa leo kinyume na barua waliyoituma halimashauri ikionyesha utekelezaji huo kutendeka.
Hata hivyo mkuu wa wilaya akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya usalama ameagiza kukamatwa kwa wahusika hao ili kufanyiwa mhojiano zaidi kwa sababu za kiusalama sambamba na kufika na vibali vinavyowaruhusu kufuga swala pamoja na hati miliki zinazoonyesha umiliki halali wa eneo hilo na kusisitiza kuwa kama hawatafanya hivyo watanyang’anywa eneo hilo na kukabidhiwa kwa mtu mwingine.
Viongozi hao waliokamatwa ni kiongozi mkuu wa miradi kutoka lake oil Fahim Mohammed na Mkurugenzi msaidizi wa lake oil Halid Mohammed, hata hivyo viongozi hao wamekana kukaidi agizo la mkuu wa wilaya na kuomba kupewa angalau muda wa mwezi mmoja kwani shughuli ya ubomoaji waliyoagizwa kufanya ni ngumu na inahitaji vifaa maalumu.
Kwa upande wake mwanasheria kutoka NEMC Manchale Heche amesema kuwa lake oil walipokea barua kutoka ofisi za NEMC ya kuwaruhusu kuendesha mradi pembezoni mwa bahari lakini hawakuruhusiwa kujenga nyumba za kudumu na walipewa masharti ambayo wameyakiuka.
Hivyo Kufuatia ukiukwaji wa masharti hayo waliyopewa kutoka NEMC mwanasheria huyo amewafutia kibali cha kuendeleza mradi huo mpaka hapo watakapokutana na kufanya makubaliano ya kupata kibali kingine na kufuata masharti kama sheria inavyosema.
0 comments:
Post a Comment