Mama mjamzito anayesadikiwa kujijeruhi
tumboni na kutoa mtoto Bi Joyce Mweupe akiwa kitandani baada ya kupokewa
na wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na kupatiwa matibabu.
Mganga Mkuunwa Mkoawa Rukwa Dkt. Boniface
Kasululu akimjulia hali mama mjamzito anayesadikiwa kujijeruhi tumboni
na kutoa mtoto Bi Joyce Mweupe akiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa
mara baada ya kupokewa na kupatiwa matibabu.
Bi Joyce Mweupe akisaidiwa kunyanyuka na
Mganaga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface kasululu akisaidiana na
muuguzi wa hospitali hiyo ya Rufaa Veronica Wambura.
Bi Joyce Mweupe akiwa na Muuguzi wa
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Veronica Wambua pamoja na Mganga Mfawidhi wa
Hospitali hiyo Dkt. John Lawi (kushoto)
………………..
Kuanzia tarehe 30 Mei, 2019 kuna taarifa
zilizosambaa na kutolewa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya
kijamii kuhusu mama mjamzito anayesemekana kujijeruhi maeneo ya tumboni
na kupelekea kutoa mtoto tumboni,tukio lililotokea katika kata ya
Kirando Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa. Baada ya kupokea
taarifa hizo timu ya ufuatiliaji iliyoundwa na wataalam wanAfya kutoka
ngazi ya Mkoa na Wilaya husika ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa
ilifanya ufuatiliaji wa tukio hilo kwa lengo la kupata uhalisia wake na
kubaini mambo yafuatayo:
1. Mhusika katika tukio hili ni Bi Joyce Mweupe Kalinda mwenye umri
wa miaka 32 anayeishi katika Kitongoji
cha Kalya, Kijiji cha Kamwanda, Kata ya Kirando, Halmashauri ya Wilaya
ya Nkasi Mkoa wa Rukwa, umbali wa takribani kilometa moja kutoka Kituo
cha
Afya Kirando. 2. Bi Joyce alipokelewa katika kituo cha Afya Kirando kilichopo katika
kata ya kirando Halmashauri ya Wilaya ya
Nkasi majira ya saa 09:30 alfajiri ya tarehe 30 Mei 2019 akiwa
amesindikizwa na ndugu zake wawili (Wifi na Shangazi yake) kwa lengo la
kujifungua ambapo alipokelewa na kufanyiwa uchunguzi wa awali.
Page 1 of 3
Katika uchunguzi huo ilibainika kuwa mama huyo alikuwa na
ujauzito unaokadiriwa kuwa na miezi tisa, akiwa na dalili za
uchungu katika hali ya kawaida kiafya. 4. Baada ya uchunguzi wa awali kukamilika alipelekwa katika wodi ya
wazazi wanaosubiri kujifungua kwa ajili ya kupumzika huku watoa
huduma wakiendelea kutoa huduma kwa wagonjwa wengine. 5. Katika ujauzito huu alikuwa akihudhuria kliniki ya Afya ya Mama
na Mtoto katika Kituo cha Afya Kirando
ambapo alifanikiwa kufanya mahudhurio matatu na hudhurio la mwisho
likiwa ni tarehe 08 Mei,
2019 6. Mnamo saa 10:30 alfajiri wakati watoa huduma wakifuatilia kujua
maendeleo yake ndipo walipobaini kuwa Bi
Joyce hakuwepo ndani ya wodi na hivyo kuanza kumtafuta katika maeneo
mbalimbali ya kituo cha afya na kutoa taarifa kwa mlinzi na uongozi wa
kituo cha
afya. 7. Wakati juhudi za kumtafuta zikiendelea, majira ya saa 12:30 asubuhi
Bi Joyce aliletwa kituoni akiwa amebebwa kwenye godoro na watu watatu (Mojawapo akiwa ni mwenyekiti wa Kijiji cha Kamwanda)
huku akivuja damu nyingi. 8. Watoa huduma walimpokea mgonjwa na kumuona akiwa
ametapakaa damu, mtoto akiwa nje ya
tumbo. Baada ya kumchunguza Bi Joyce alibainika kuwa na jeraha
lilililosababishwa na kitu chenye ncha kali tumboni huku sehemu ya
utumbo, mfuko wa uzazi, kondo la nyuma na mtoto vikiwa nje na yeye
mwenyewe akiwa hajitambui. Baada ya hapo timu ya Kituo cha Afya
ikongozwa na Mganga Mfawidhi Dkt. Gideon Msaki iliendelea na huduma za
upasuaji wa dharura kwa ajili ya kuokoa Maisha ya Bi Joyce.
Baada ya huduma za upasuaji wa dharura
kufanyika timu ya ufuatiliaji iliendelea na ufuatiliaji zaidi wa tukio
hili na kubaini ifuatavyo:
1. Bi Joyce alipotoka kituo cha Afya alirudi nyumbani kwake
anapoishi yeye,mtoto wake wa kiume aitwaye Linus Sindani
Page 2 of 3
anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 12 au 13 na mume
wake ambaye siku ya tukio hakuwepo nyumbani. 2. Mara baada ya kurudi nyumbani Bi Joyce alimwagiza mwanaye
(Linusi) kwenda kumuita shangazi yake
ambaye anaishi maeneo ya jirani na nyumbani kwao. Waliporudi wakiwa na
shangazi ndipo walipomkuta Bi Joyce akiwa ameloa damu na hivyo kutoa
taarifa kwa majirani na mwenyekiti wa Kijiji kwa ajili ya msaada
zaidi. Hitimisho
1. Timu ya ufuatiliaji imejiridhisha kuwa huduma za dharura za
upasuaji wa kuokoa Maisha ya Bi Joyce
zimefanyika kwa mafanikio makubwa katika kituo cha Afya Kirando na
kwamba mama na mtoto ambao kwa sasa wamehamishiwa katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa
kwa uangalizi zaidi wanaendelea vizuri 2. Tunatoa pongezi kubwa kwa watumishi wa Kituo cha Afya Kirando
kwa juhudi kubwa walizofanya kuokoa
Maisha ya Bi Joyce Kalinda. 3. Tukio hili limeripotiwa katika jeshi la
Polisi kwa ajili ya kuendelea na uchunguzi zaidi.
0 comments:
Post a Comment