Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini Mh Fabian Daqaro amezitaka kaya maskini katika jiji la Arusha zinazonufaika na Fedha za TASAF awamu ya tatu kuzitumia vizuri ili ziwanufaishe na kuwainui kiuchumi.
Akizungumza na wananchi waliofaidika na mpango huo wa Tasaf kata ya Sombetini na Daraja mbili amesema kuwa ni vema fedha hizo zikawasaidie kwa kuanzisha biashara ndogo ndogo kufanya ufugaji na kuweka akiba ya baadae.
“Serikali inataka wananchi wote waishi maisha mazuri lakini haina huo uwezo kwa mara moja cha msingi kwa sisi ambao tumebahatika nah ii Program ya TASAF awamu ya tatu hizi pesa tukazitumie vizuri ukichukua elfu 20 ukaenda kununua kanga sasa wewe utakuwa unatusaliti lakini nenda kanunue nyanya,kama ni mboga za majani fanya biashara zitakusaidia kwenye maisha yako”Alisema Dc Daqaro
Hata hivyo Daqaro amewasisita wataalamu wa maendeleo ya jamii na wenyeviti wa mitaa pamoja na watendaji kuwasaidia wananchi kwa kupita kwa kuwa karibu nao na kuwasilkiliza ili shida zao zitatuliwe mapema zaidi na kwa wakati.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi walionufaika na mpango huo wa Tasaf Bi Monica Thomas amemshukuru mkuu wa wilaya kwa kuwatembelea na kuwakabidhi fedha hizo na amemuomba afikishe salamu kwa Raisi Magufuli kwa kuwajali maskini.
Amesema kuwa fedha hizo zimewasaidia kwa kuwa wamepata mitaji na kuanzisha biashara kama mama ntilie na kufuga kuku hivyo kwasasa wana uwezo wa kupata milo mitatu na kuwapeleka watoto shule.
Naye mratibu wa TASAF jiji la Arusha Bi Tajiel Mahega amesema kuwa mpango huo ni kwa ajili ya mitaa 70 ambapo wamefikia kaya 4773 na zaidi ya shilingi milioni 100 zimetolewa.
0 comments:
Post a Comment