Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari
(MAELEZO), Rodney Thadeus akizungumza na Maafisa Habari na Mawasiliano Serikali
wakati wa mafunzo kuhusu mwongozo wa uandishi wa tovuti za Mikoa na Mamlaka ya
Serikali za Mitaa yaliyofungwa leo Ijumaa Machi 23, 2018 Mkoani Morogoro.
Mafunzo hayo yaliandaliwa na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3)
kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia ufadhili wa Shirika la
Misaada la Marekani (USAID).
Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakifuatiliano mafunzo mafunzo kuhusu mwongozo wa uandishi wa tovuti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa yaliyofungwa leo Ijumaa Machi 23, 2018 Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Afisa Habari kutoka Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Atley Kuni akizungumza na Maafisa Habari na Mawasiliano Serikali wakati wa mafunzo kuhusu mwongozo wa uandishi wa tovuti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa yaliyofungwa leo Ijumaa Machi 23, 2018 Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Na
Mwandishi Wetu, Morogoro
MAAFISA Habari na
Mawasiliano katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa
nchini, wametakiwa kuongeza kasi ya matumizi ya
mitandao ya kijamii ikiwemo tovuti ili kuleta mageuzi yaliyokusudiwa na Serikali katika
kutangaza shughuli za maendeleo ya wananchi.
Hayo yamesemwa leo (Ijumaa
Machi 23, 2018) Mkoani Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari
(MAELEZO), Rodney Thadeus wakati wa kufunga mafunzo ya siku nne kwa Maafisa
Habari na Mawasiliano Serikalini yaliyohusu mwongozo wa uendeshaji wa Tovuti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za
Mitaa nchini yaliyoandaliwa na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma
(PS3) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia Ufadhili wa Shirika la
Misaada la Marekani (USAID).
Thadeus alisema
Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Wakala ya Serikali Mtandao (EGA) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3)
kwa pamoja waliandaa mwongozo huo ili kuhakikisha kuwa tovuti za Mikoa na
Halmashauri zinakuwa nyenzo muhimu ya taarifa za Serikali.
“Mafunzo mliyoyapata ni
vyema mkahakikishe kuwa tovuti zenu zinaweza kusaidia maendeleo ya wananchi kwa
kutangaza shughuli za maendeleo pamoja na kuzingatia thamani ya fedha
zilizotolewa na wadau wetu wa maendeleo kwa kuleta mabadiliko ya mwonekano wa
tovuti zetu” alisema Thadeus.
Aidha alisema kupitia
mafunzo yaliyotolewa kuhusu mwongozo huo, ni matarajio ya Serikali kuwa tovuti
zote za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zitakuwa zimesheni habari
zilizoandikwa kwa usahihi pamoja na kuwekwa taarifa za mara kwa mara hatua
itayowezesha wananchi wengi Zaidi kuweza kuzitembelea na kupata huduma
zinazostahili.
Alisema Ofisi yake ipo
tayari kufanyia kazi na Maafisa Habari na Mawasilino waliopo katika Mikoa na
Mamlaka za Serikali za Mitaa iwapo kutajitokeza changamoto yoyote inayohusu
usimamizi, uendeshaji na uboreshaji wa maudhui ikiwemo mafunzo ya mara kwa mara
kwa watendaji wa tovuti hizo.
Thadeus alisema Idara
ya Habari (MAELEZO) itahakikisha kuwa inafanya mawasiliano ya mara kwa mara na
Watendaji Wakuu wa Mikoa na Halmashauri za Wilaya ili kuhakikisha kuwa Maafisa
Habari na Mawasiliano ambao ndio watendaji
wa tovuti hizo wanapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Wakuu
mbalimbali wa Idara na Vitengo katika Mikoa na Halmashauri zote nchini.
Kwa upande wake, Afisa
Habari kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Atley Kuni alisema malengo ya Serikali ni
kuhakikisha kuwa tovuti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakuwa
kiunganishi baina ya Serikali na wananchi kwa kuhakikisha zinatangaza taarifa
mbalimbali za mafanikio ya Serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Tumepanga tuwe na
jarida maalum litakalokuwa na habari mbalimbali za mafanikio ya miradi ya
maendeleo, ambazo zitakuwa zikiandikwa na Maafisa Habari na Mawasiliano waliopo
katika Mikoa na Halmashauri ambazo zitakuwa zikiakisi maendeleo yaliyoweza
kupatikana mara baada ya kuanzishwa kwa tovuti hizi” alisema Kuni.
Aidha aliongeza kuwa
Maafisa Habari na Mawasiliano wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa hawana
budi kuongeza ubunifu ili kuhakikisha kuwa tovuti hizo pia zinaweza kuwa chanzo
kikuu cha mapato katikas maeneo yao ya kazi.
0 comments:
Post a Comment