Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini akisisitiza jambo wakati akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano wake katika Kijiji cha Kasaka Kata ya Igulwa Mkoani Geita, Jana 3 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini katika Kijiji cha Kasaka Kata ya Igulwa Mkoani Geita wakati akiwa katika ziara ya jimbo kukagua shughuli za maendeleo, Jana 3 Machi 2018.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini katika Kijiji cha Kasaka Kata ya Igulwa Mkoani Geita wakati akiwa katika ziara ya jimbo kukagua shughuli za maendeleo, Jana 3 Machi 2018.
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Nampangwe kilichopo katika Kata ya Runzewe Mashariki Mkoani Geita wakifatilia mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini wakati akiwa katika ziara ya jimbo kukagua shughuli za maendeleo, Jana 3 Machi 2018.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini akishiriki ujenzi wa madarasa ya shule ya Kata ya Igulwa Mkoani Geita baada ya mkutano wa hadhara wa wananchi Jimboni Bukombe waliohudhuria mkutano wake katika Kijiji cha Kasaka , Jana 3 Machi 2018.
Na Mathias Canal,
Geita
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye ni
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini, ameunga mkono jitihada za wananchi
walizozifanya katika ujenzi vyumba vitano vya madarasa kwa ajili ya Shule ya
sekondari ya Kata ya Igulwa kwa kuchagia jumla ya mabati 279 kwa ajili ya
kupaua majengo hayo.
Biteko ameunga mkono juhudi hizo za wananchi kwa kuchangia
shilingi milioni 2.3 huku jumla ya shilingi milioni 4.4 zikitolewa na wadau wa
maendeleo katika Jimbo la Bukombe ambazo zote kwa pamoja zitawezesha upatikanaji
wa mabati hayo.
Ametoa mchango huo Mara baada ya kuzuru katika Kijiji cha Kasaka
kwa ajili ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo akiwa katika ziara ya kijimbo kwa
kukutana na wananchi kwa kufanya mikutano ya hadhara yenye lengo la kuelezea
jinsi serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt
John Pombe Magufuli ilivyojipanga kuwanufaisha wananchi kupitia rasilimali zao
yakiwemo madini.
Alisema kuwa pindi ujenzi wa shule hiyo ya sekondari
utakapokamilika utawarahisishia wanafunzi kupata huduma za elimu kirahisi
kutokana na adha waliyoipata katika kipindi kirefu katika kuitafuta elimu kwa
kuhimili mwendo mrefu.
Mhe Biteko aliwataka wananchi kumuunga mkono Rais Magufuli kwa
kumuombea katika Vita kubwa anayokabiliana nayo hususani katika kuimarisha
uchumi wa mtu mmoja mmoja sambamba na Taifa kwa ujumla wake.
Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kumlaki katika
mkutano wa hadhara uliofanyika Katika kijiji cha Nampangwe kilichopo katika
Kata ya Runzewe Mashariki Mhe Biteko amechangia pia mabati 95 yenye thamani ya
shilingi milioni 2.28 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya
Runzewe Mashariki.
Sambamba na hayo pia aliunga mkono juhudi za wananchi hao kwa
kuchangia mifuko 100 ya saruji ambapo mifuko 50 itatumika kwa ajili ya
uendelezaji wa ujenzi wa zahanati huku mifuko mingine 50 ya saruji akitoa kwa
ajili ya ujenzi wa choo cha shule hiyo.
Mbunge wa Jimbo hilo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye
ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Leo 5 Machi 2018 amemaliza ziara ya Siku
Tatu ya kijimbo aliyoanza 3 Machi 2018 ambapo pamoja na mambo mengine amefanya
jumla ya mikutano mitatu ya ndani, mikutano mitano ya hadhara, amekagua
shughuli za maendeleo ya wananchi sambamba na kuchangia utatuzi wa kero mbalimbali
za wananchi katika sekta ya elimu, afya na barabara.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment