Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi wa Kijijini cha Kazilamuyaye, Kata ya Runzewe Magharibi Leo 4 Machi 2018, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu Jimboni humo. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kazilamuyaye, Kata ya Runzewe Magharibi Wilayani Bukombe wakimsikiliza kwa weledi Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo, Leo 4 Machi 2018.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi wa Kijijini cha Kazilamuyaye, Kata ya Runzewe Magharibi Leo 4 Machi 2018, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu Jimboni humo.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kazilamuyaye, Kata ya Runzewe Magharibi Wilayani Bukombe wakimsikiliza kwa weledi Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo, Leo 4 Machi 2018.
Na Mathias Canal, Geita
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ameitaka Taasisi ya kuzuia na
kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza kiasi cha shilingi milioni 3.9
kilichotolewa na mfuko wa Jimbo katika Kata ya Runzewe Magharibi kimetumika
katika kazi gani.
Mhe Biteko ametoa agizo hilo Leo 4 Machi 2018 Kijijini Kazilamuyaye wakati akihutubia
wananchi waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya ukaguzi
wa shughuli za maendeleo Jimboni kwake sambamba na kukutana na wananchi ili
kubaini matatizo yanayowakabili.
Mbunge Biteko ametoa kauli ya uchunguzi huo Mara baada ya
wananchi kulalamikia kukosekana fedha za ujenzi wa shule ya msingi Kazilamuyaye
huku wanafunzi wakikumbana na kadhia mbalimbali kutokana na kukosekana kwa shule
ya msingi katika eneo hilo.
Alisema kuwa serikali kupitia mfuko wa Jimbo ilitoa fedha hizo
kwa ajili ya kuchagiza ujenzi wa majengo ya shule hiyo sambamba na ujenzi wa
choo jambo ambalo kwa muda mrefu halijatimizwa huku ikielezwa kuwa fedha hizo
zimebwinywa na aliyekuwa msimamizi wa ujenzi huo.
"Ndugu zangu nataka niwakumbushe kuwa mnaweza kula fedha
zote mtakazo lakini fedha za Rais Magufuli zikielekezwa mahala inapaswa kufanya
kazi husika endapo ikibadilishiwa matumizi lazima wahusika wachukuliwe
hatua" Alikaririwa Mhe Biteko wakati akizungumza na wananchi hao
Katika hatua nyingine ili kuendeleza ujenzi wa shule hiyo ili
kurahisisha wanafunzi kupata elimu kwa ukaribu ili kukinzana na changamoto
wanazokabiliana nazo kutokana na umbali wa shule ambapo Mbunge Biteko
amechangia mabati 70 sambamba na mifuko 50 ya saruji.
Kuhusu Kero ya zahanati iliyoelezwa na wananchi hao wakati wa
mkutano, Mhe Biteko amewaeleza wananchi kuwa serikali imetoa shilingi milioni
333.9 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho cha Kazilamuyale
huku Mbunge huyo akichangia mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya shughuli hiyo.
Katika hatua nyingine Mhe Biteko amewataka wananchi kushiriki
kwa hali na Mali pindi utakapoanza ujenzi wa zahanati na shule ya msingi Kazilamuyaye
badala ya kuacha jukumu hilo kwa serikali pekee.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko anaendelea na
ziara ya siku tatu ya kijimbo ambapo pamoja na mambo mengine anasikiliza Kero
za wananchi ikiwa ni pamoja na kukagua shughuli za maendeleo.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment