1. WAZIRI wa Nchi,
Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa jimbo la Bahi Omary
Badwel na viongozi wengine wa wilaya ya Bahi.
Daraja la Chipanga
linaloendelea kujengwa
Mtendaji Mkuu wa
TARURA Mhandisi Victor akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa ujenzi wa daraja la
Chipanga.
..............................................................
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo amemtaka
mkandarasi wa kampuni ya Medes Company Limited na Millenium Master Builders (T)
Limited anayejenga daraja la Chipanga wilayani Bahi, kukamilisha ujenzi wa
daraja hilo ifikapo mwezi Julai, mwaka huu bila visingizio vyovyote.
Akikagua ujenzi wa daraja hilo, Jafo amesema awali kazi ya
ujenzi wa Daraja hilo ilitarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu
lakini kutokana na Mvua zilizokuwa zikinyesha amewaelekeza kukamilisha ifikapo
Julai mwaka huu.
Jafo amewaagiza wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA)
kukaa na mkandarasi kukubaliana tarehe ya mwisho ya kukamilika kazi hiyo lakini
kinachotakiwa ifikapo Julai mwaka huu daraja hilo liwe limekamilika.
Amebainisha kuwa daraja hilo ni kiunganishi cha kata ya Chipanga
na Makao makuu ya wilaya ya Bahi na ujenzi wake unagharimu kiasi cha Sh.
bilioni 2.11.
Akizungumza katika mkutano wa hadharana wananchi wa Chipanga, Waziri Jafo amewataka
wananchi hao kuacha tabia ya kupitisha ng'ombe na majembe ya ng’ombe kwenye barabarani
zinazojengwa kwa kuwa wanasababisha uharibifu wa barabara.
Amesema serikali haiwezi kuvumilia uharibifu wowote wa
miundombinu ambayo inagharimu gharama kubwa.
0 comments:
Post a Comment