Pichani ni mifuko ya saruji iliyotolewa na mkuu wa wilaya ya
Ikungi Miraji Mtaturu kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya walimu katika
shule ya Sekondari ya Dadu.
Katibu tawala wa wilaya ya Ikungi Winfrida Funto akikabidhi
mifuko ya saruji kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Miraji Mtaturu kwa
ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya walimu katika shule ya sekondari ya
Dadu,wa kwanza kushoto Afisa Elimu wilaya Jonah Katanga,Mkuu wa shule hiyo
Imani Mbegezi na mwanafunzi Daud Robert.
Katibu Tawala wa wilaya ya Ikungi Winfrida Funto akikabidhi
mifuko ya saruji kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Miraji Mtaturu kwa
ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya walimu katika shule ya sekondari ya
Dadu,wa kwanza kushoto Afisa Elimu wilaya Jonah Katanga,mkuu wa shule hiyo
Imani Mbegezi na mwanafunzi Daud Robert.
......................................................................................................
MKUU wa wilaya ya Ikungi mheshimiwa Miraji Mtaturu ametekeleza ahadi yake aliyoitoa wiki iliyopita ya kusaidia mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ofisi ya walimu katika shule ya sekondary ya Dadu iliyopo wilayani humo.
Ukamilikaji wa ofisi hiyo utasaidia walimu hao kupisha darasa wanalotumia kama ofisi liweze kutumiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza.
Akikabidhi mifuko hiyo ya saruji kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo kwa Mkuu wa shule,Katibu Tawala wa wilaya hiyo Winfrida Funto ametoa wito kwa uongozi wa shule kujitahidi kukamilisha ofisi hiyo mapema ili wapishe darasa litumiwe na wanafunzi ili kupunguza upungufu wa vyumba vya madarasa uliopo shuleni hapo.
Ahadi ya mkuu huyo wa wilaya aliitoa alipotembelea shule hiyo na kujionea changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa madarasa na ukosefu wa maabara.
Kufuatia changamoto hizo mheshimiwa Mtaturu aliahidi kuchangia pia mifuko 100 kwa ajili ya kujenga maabara ambapo serikali ilichangia shilingi milioni 5 zilizonunuliwa matofali yapatayo 1,500 lakini hawakuendelea kujenga toka mwaka 2014.
Katika ziara yake shuleni hapo aliyoifanya wiki iliyopita mbali na ahadi aliyoitoa aliiagiza bodi ya shule na uongozi wa kata kuhamasisha wananchi kuchangia nguvu kazi kwa kusogeza mchanga,maji na kuchimba msingi.
0 comments:
Post a Comment