Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza katika hafla ya ugawaji wa kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza katika hafla ya ugawaji wa kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akigawa kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.
Wanafunzi wakiwa katika hafla ya ugawaji wa kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akikabidhi kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akikabidhi kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma akiwa na vion.ozi mbalimbali.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akikabidhi kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma akiwa na vion.ozi mbalimbali.
.............................................................................................................
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amempongeza
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) kwa kazi kubwa anayofanya ya
kuwaletea wananchi maendeleo hasa katika kuboresha sekta ya Elimu jimboni humo.
Ulega ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya ugawaji wa kompyuta
kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere
Square-Dodoma.
Kompyuta hizo 22 zenye thamani ya Sh. Milioni 44 na zimetolewa
na Mbunge Mavunde pamoja na wadau wa maendeleo katika kusaidia kuboresha sekta
ya Elimu jimboni hapo.
Naibu Waziri Ulega amesema kwa sasa Dodoma ni Makao Makuu hivyo
Mavunde anapaswa kupongezwa kwa jitihada zake katika sekta ya elimu.
Ulega ambaye ni Mbunge wa Mkuranga amesema kuna
baadhi ya wazazi hawajawahamisha watoto wao Mkoani humo kutokana na uhaba
wa shule hivyo kupitia jitihada za Mbunge huyo shule zitaongezeka na
idadi ya wanafunzi itakuwa kubwa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mavunde ameahidi kuzipatia
kompyuta shule zote 130 na kuahidi kuboresha miundombinu ya nishati katika
shule zote ili wanafunzi wengi zaidi wapate nafasi ya kujifunza kwa kutumia
teknolojia ikiwa ni muendelezo wa ugawaji wa vifaa vya kieletroniki katika
mashule ambao ulitanguliwa na ugawaji wa vishkwambi (tablets)500 zenye thamani
ya Sh.Bilioni 1.
Amesema
Jimbo lake lina upungufu wa madarasa 1038 hivyo kwa kupitia mfuko wa
Jimbo atatoa sh.milioni 55 ambazo zitatumika kufyatua matofali ili kupunguza
upungufu huo.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Kaimu Mkuu wa Wilaya wa Dodoma Mjini
ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratias Ndejembi ameahidi kushirikiana na Mbunge kutatua
changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu ili kuhakikisha kuwa
wanafunzi wanapata elimu bora katika mazingira rafiki.
0 comments:
Post a Comment