METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, February 22, 2018

Mhe Mwanjelwa apongeza Watafiti kutoa majibu ya matatizo ya Wakulima



Na Wazo Huru Blog

Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa amewapongeza Watafiti wa Tanzania kwa kusaidia kubuni wazo la utafiti masuala ya kilimo nchini yanayolenga kuboresha mambo ya Sera za Kilimo, Usalama wa Chakula na Kuongeza Tija katika uzalishaji mbegu za mazao ya nafaka na yale ya jamii ya mikunde.

Dkt. Mwanjelwa amesema utafiti huo utumia mikakati ya kisayansi kupima uhalisia wa matumizi ya mbegu bora miongoni mwa Wakulima.

Ameongeza kuwa mikakati hiyo ya kisayansi ni pamoja na kuchukua sampuli ya mazao husika kabla ya kuvunwa na kuzipima katika maabara ili kubaini vinasaba vya mbegu zinazopandwa na Wakulima na kuongeza kuwa matokeo ya utafiti huo yametoa takwimu za kuaminika kwa lengo la kuongeza tija itokanayo na matumizi ya mbegu bora na hivyo kufanya kilimo cha Tanzania kuwa wa uhakika.

“Nimedokezwa kuwa, utafiti huu wa aina yake, umeangalia mazao makuu manne; Mahindi, Mpunga, Maharage na Muhogo. Mazao haya ni kati ya mazao 15 yaliyopewa kipaumbele kwenye Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili yaani (ASDP II) Programu ambayo tunataraji kuizindua kuanza hivi karibumi”. Amekaririwa Dkt. Mwanjelwa.

Naibu Waziri ameongeza kuwa matokeo ya utafiti huu yatagusa mambo yanayoangaliwa duniani kwa sasa pamoja na kuweka mkazo kwenye uhakika na usalama wa chakula, pamoja na masuala ya lishe.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa amewashukuru Wawakilishi wa Mfuko wa Wakfu wa Bill na Melinda Gates kwa kufadhili Mradi huo wa Utafiti.

MWISHO
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com