Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na
walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Mwandege.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na
walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Mwandege.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akitoa maagizo kwa
viongozi wa wilaya ya Mkuranga juu ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi
Mwandege.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua matofali
yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa shule mpya ya Kipara Mpakani.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mwandege wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipo watembelea shuleni hapo.
....................................................................
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Mkuranga na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuanza ujenzi wa madarasa haraka
iwezekanavyo katika shule ya msingi Mwandege ili kuondoa msongamano wa wanafunzi
madarasani.
Agizo hilo amelitoa leo baada ya kutembelea katika Shule hiyo
yenye zaidi ya wanafunzi 3700 ambapo kati yao wanafunzi zaidi ya 560 ni darasa
la kwanza pekee.
Amesema kutokana na hamasa kubwa ya jamii kuwapeleka watoto
kujiunga na elimu ya msingi kwa kutumia fursa ya elimu ya msingi bila malipo
kumesababisha msongamano wa wanafunzi shuleni hapo.
Aidha Waziri Jafo amewaangiza viongozi hao wa wilaya kuweka mikakati
ya haraka ili kuondoa kero ya vyumba vya madarasa na madawati shuleni hapo.
Kadhalika, Jafo ameagiza ujenzi wa shule mpya katika eneo la
Kipara Mpaka ambalo lipo jirani na shule ya mwandege sambamba na
kukamilisha shule mpya ya Chatembo ili kupunguza idadi kubwa ya wanafunzi
waliopo kwenye shule hiyo.
Amesema baada ya shule hizo kujengwa wanafunzi hao watatawanywa katika
maeneo hayo mapya.
Katika kupunguza kero hiyo ya upungufu wa nyumba vya madarasa, Waziri Jafo amewapa hamasa walimu kwamba
serikali itapeleka fedha ndani ya wiki hii ili ujenzi wa vyumba vitatu vya
madarasa uanze haraka iwezekanavyo.
“Ifikapo Machi 6, mwaka huu vyumba vya madarasa viwe
vimekamilika na nawaonya Ofisi ya mkuu wa wilaya na Ofisi ya mkurugenzi kuacha
malumbano yasiyo na maana ambayo yanarudisha nyumba upelekaji wa huduma za
jamii kwa wananchi,”amesisitiza Jafo
Katika ziara hiyo, Jafo amewaomba viongozi na wananchi wa wilaya ya
Mkuranga wamuunge mkono Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Abdallah Ulega kwani
anajituma sana kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkuranga.
0 comments:
Post a Comment