Na Beatrice
Kimwaga, Wizara ya Kilimo-Lindi
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary
Mgumba amewasihi wakulima nchini kulima kwa wingi kilimo cha muhogo kwani
kufanya hivyo kutaimarisha kipato chao.
Mgumba ameyasema hayo mara baada ya kutembelea
Kiwanda cha kuchakata Muhogo kilichopo katika kijiji cha Mbalala kata ya Mtama
katika Halmashauri ya Lindi wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani
Lindi.
Katika ziara hiyo Mhe Mgumba
alikipongeza kiwanda cha Cassava Starch of Tanzania Corporation ( CSTC) kwa
kutoa ajira nyingi kwa watanzania walio wengi katika wilaya hiyo sambamba na
kuwapongeza kwa uamuzi wao mzuri wa kuwekeza nchini.
Alisema kuwa wawekezaji hao wameunga
mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli katika azma yake ya kufanya Tanzania kuwa
nchi ya Viwanda.
“Kuwepo kwa kiwanda hiki kuna faida
kubwa kwani kitatengeneza ajira kwa wananchi kupata soko la muhogo, uzuri ni
kwamba kiwanda hiki kitatumia malighafi zinazozalishwa hapa Tanzania na sio nje
ya nchi” alisema Mhe. Mgumba
Alisema kuwa pamoja na mambo mengine
lakini changamoto kubwa iliyopo ni uwepo wa tija ndogo katika mazao yetu hivyo uwepo
wao nchini utasaidia wananchi kujifunza na kupata teknolojia mpya waliyokuja
nayo na teknolojia hiyo itasambaa Lindi nzima.
Kwa upande wa wamiliki wa kiwanda
hicho wamesema kwamba lengo lao ni kuzalisha tani elfu sitini na kwa upande wa
Serikali Mhe. Mgumba amesema imejipanga
kwenda kwenye uchumi wa kati ifikapo 2020.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya
tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kuimarisha
masoko ya mazao ya wakulimahivyo wakulima jukumu lao kubwa ni kuongeza
uzalishaji na tija katika kilimo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment