METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, January 26, 2018

WAZIRI WA AFYA ARIDHISHWA NA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KARUME ILEMELA

Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe Ummy Mwalimu ameridhishwa na ujenzi wa kituo cha afya cha Karume kilichopo wilaya ya Ilemela kata ya Bugogwa kilichozingatia masharti ya fedha zilizotolewa kwaajili ya ujenzi huo

Mhe Ummy Mwalimu ameyasema hayo alipofanya ziara katika kituo hicho cha afya kukagua miundombinu ya kituo hicho na utoaji wa huduma ambapo amesema

'... Nimefurahi kuona zile shilingi milioni mia tano zilizoletwa hapa zimetumika vizuri, Na zile fedha ni kwaajili ya kujenga chumba cha upasuaji, Wodi ya wazazi, Jengo la maabara ya damu na Nyumba ya mtumishi, Lakini tukasema kama fedha zitabaki mnaweza kujenga majengo mengine, Sasa hapa nmefurahi sana kwa kazi iliyofanywa na wilaya ya Ilemela hongereni sana sana ..'

Aidha Waziri huyo wa afya amemuahidi Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula kuleta fedha nyengine kwaajili ya kituo cha afya cha Buzuruga kufuatia kuridhishwa kwake na usimamizi mzuri wa shughuli za maendeleo anaoufanya pamoja na kuwaagiza wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanatumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amempongeza Waziri huyo wa afya kwa namna anavyosimamia utekelezaji wa majukumu ya wizara yake nakumshukuru kwa msaada wa gari la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa kwa wilaya ya Ilemela mapema mwaka wa Jana, Huku akimuomba kufikisha salamu za wana Jimbo la Ilemela kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Magufuli kwa namna anavyowajali wananchi wa Ilemela huku akiahidi kusimamia fedha zozote za maendeleo zitakazoletwa ndani ya Jimbo lake

Akimkaribisha Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela amefafanua juu ya miradi mbalimbali ya afya inayotekelezwa na itakayotekelezwa ndani ya mkoa wake pamoja nakuwaomba viongozi na wananchi kuunga mkono jitihada za utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano katika mkoa huo

' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
26.01.2018

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com