MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amemtaka Katibu Tawala wa mkoa
huo, Richard Kwitega kufuatilia aliyetoa taarifa ya uongo kwenye kikao
cha Kamati ya Ushauri ya mkoa wa Arusha kuhusu Halmashauri ya wilaya ya
Ngorongoro kutokuwa na upungufu wa madawati kabisa.
Alitoa agizo hilo baada ya taarifa iliyokuwa ikitolewa na Ofisa Elimu
Taaluma Mkoa wa Arusha, Nestory Mroka kumshangaza yeye na baadhi ya
wajumbe wa kikao hicho kutoka wilayani Ngorongoro wakiongozwa na Mkuu wa
wilaya hiyo, Mfaume Taka na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mathew
Siloma.
Alisema alifanya ziara Ngorongoro na kujionea hali halisi ya upungufu
wa madawati na kutoa maagizo kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
(NCAA) kuhakikisha inakamilisha ahadi ya kuchangia madawati 2,000.
“Hizi taarifa umezipata wapi na kwa nini useme Ngorongoro haina uhaba
wa madawati wakati nimefanya ziara mwenyewe na kujionea hali halisi,
naomba RAS (Katibu Tawala) ufuatilie hii taarifa ya madawati ili kujua
ni nani ameitoa nichukue hatua stahiki … naomba ufuatilie hii taarifa
ili kubaini ni nani ameileta hapa kwa sababu ni ya uongo…Ngorongoro ina
upungufu wa madawati na nyie mnasema hakuna, hapana hii taarifa
inadanganya,” alisema.
Mashaka ya Gambo dhidi ya taarifa hiyo yaliungwa mkono na Mkuu wa
Wilaya ya Ngorongoro aliyesema wilaya yake ina upungufu mkubwa wa
madawati na baadhi ya wanafunzi wanakaa chini, hivyo hafahamu ni kwa
nini taarifa hiyo inasomwa kuwa hakuna upungufu wa madawati.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Siloma alisema hadi hivi sasa NCAA imetoa madawati 500 tu kati ya yaliyoahidiwa.
Saturday, October 22, 2016
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. ...
-
Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel Jeremia Opulukwa akinawa mikono kabla ya kuingia katika Zahanati ya Saza itakayotumika kutibu endapo ata...
-
MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Tanzania (DCI), Robert Boaz Mikomangwa amesema Jeshi la Polisi nchini Tanzania na vyombo vingi...
-
Naibu waziri Kilimo Mhe. Omari T. Mgumba (Mb) akiwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa arusha alipokutana na wataalamu wa kilimo ,ushirika na ...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment