Wazee wa Kata ya Nyamanoro Jimbo la Ilemela wamemtuma Mbunge wao na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula kupeleka salamu za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Magufuli kwa jitihada kubwa anazozifanya katika kuwaletea maendeleo.
Akizungumza kwa niaba ya wazee hao mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya Ibungilo Ndugu Dotto Erasto Mangu amesema kuwa wazee wa Nyamanoro wanaridhishwa na jitihada kubwa zinzofanywa na Mhe Rais katika kulitumikia Taifa hasa udhibiti wa mianya ya upotevu wa rasilimali za nchi ikiwemo mapato na madini, utekeleaji wa miradi mikubwa ya ujenzi wa reli ya kisasa, ununuzi wa ndege mpya na za kisasa, upanuzi wa uwanja wa ndege wa mkoa Mwanza na barabara yake ya kutoka mjini kati kwenda uwanja wa ndege inayopita katika kata yao, kurudisha nidhamu ya kazi kwa watumishi wa Umma, uboreshaji wa huduma za afya na ongezeko la bajeti yake
‘… Mheshimiwa mbunge wazee wa Nyamanoro wanasalamu zao tunakuomba uzipeleke kwa Mheshimiwa Rais John Magufuli, Kamwambie tunamshukuru sana kwa kututetea sisi wanyonge lakini pia jitihada anazozifanya za kulijenga taifa hili, Kasi yake inaonekana wala haijifichi na tunampongeza kwa hekima anazozitumia katika kukisaidia chama chetu leo tunaona wapinzani wanavyomiminika kurudi kwetu, CCM wanaiamini wananchi, Wenyewe mmeona kupitia uchaguzi huu mdogo uliokwisha majimbo yote tumeshinda kwa zaidi ya 90%…’ Alisema
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Dkt Angeline Mabula amewahakikishia wazee hao kuzifikisha salamu hizo huku akiwaomba kuendelea kumuombea na kumuunga mkono Mhe Rais na wasaidizi wake na kuwataka kuwa wazalendo kwa kulitumia vizuri zoezi la urasimishaji makazi litakalofika ukomo mwezi Juni 30, 2018 kwa kulipia upimaji na hati miliki
Mbunge wa Ilemela amehitimisha ziara yake ya utekelezaji wa Ilani kwa kata hiyo ya Ibungilo ziara iliyohusisha jumla ya kata 14 za Kayenze, Sangabuye, Bugogwa,Shibula, Kahama, Buswelu, Nyamhongolo, Nyakato, Mecco,Buzuruga, Nyasaka, Kawekamo na Ilemela, kwa awamu ya kwanza, Na kuahidi kumalizia kata 5 zilizobaki kufikisha jumla ya kata zote19 za Jimbo lake mara baada ya kumalizika kwa vikao vya uwakilishi bungeni mjini Dodoma.
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
16.01.2018
0 comments:
Post a Comment