Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ameyasema hayo wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika Manispaa ya Ubungo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kwa kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM 2015-2020 na kamati ya Siasa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Ziara hiyo ni ya siku mbili ambayo imeanza rasmi leo tarehe 16/01/2016 inayohusisha wajumbe 10 wa kamati ya Siasa Wilaya ya Ubungo.
Lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa katika Manispaa ya Ubungo kwa kipindi cha mwaka 2016/2017 ambayo ilani ya Ccm ya 2015-2020 imeelekeza kwa kuzingatia Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM ambacho ni chama Dola.
Wajumbe wa kamati hiyo ya Siasa wamedhuru katika Wilaya ya Ubungo wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg Lucas M. Mgonja na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makore
Kabla ya Ziara waliambatana na Mkuu wa wilaya ya Ubungo na kufanya mazungumzo ya awali na wakuu wa Idara na Vitengo katika ukumbi wa Manispaa Makao makuu ulioko kibamba CCM.
Ujumbe huo ulibanisha wazi kuwa kwa kuzingatia Ilani 229 na 230 Katiba Ibara ya 76 wanatakiwa kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kujionea uhalisia wa miradi hiyo hivyo watendaji ambao ni wakuu wa Idara watoe ushirikiano pasina shaka.
Kamati hiyo kwa siku ya leo imefanikiwa kutembelea miradi minne (4) ya Maendeleo ambayo ni mradi wa maji Hondogo kata ya kibamba, Daraja la mbezi kwa Londa.
Pia ujenzi wa choo cha matundu 12 shule ya msingi Makabe na ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Kimara
Aidha Kayombo amehikikishia kamati hiyo kuwa yeye ni muumini mzuri wa Ilani ya CCM pamoja na wakuu wote wa Idara na vitengo atahakikisha anaendana na kasi ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Mhe. Rais *Dr John Pombe Magufuli
Karibu Ubungo ziara inaendelea kesho tarehe 17/01/2018 kwa pamoja tuijenge Ubungo.
Imetolewa na :
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
0 comments:
Post a Comment