METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, September 1, 2017

AJALI YA GARI YASABABISHA MTU MMOJA KUFARIKI NA KUJERUHI 9 MAKETE-NJOMBE

Ajali hiyo imetokea usiku wa Kuamkia jana kijiji cha Lupalilo ambapo gari aina ya ROSA Mali ya Kampuni ya Japanese,gari hiyo ilikuwa imetokea Mbeya kuelekea Ikonda ilipunduka na kusababisha kifo cha Mwanamke mmoja

Sababu za ajali hiyo bado hazijatolewa lakini inasemekana kuwa ilikuwa kwenye Mwendo mkali mteremkoni na kufeli breki huku Dereva akishindwa kulimudu

Taratibu za Mazishi zikiendelea kwa aliyepoteza Maisha na Majeruhi tisa wamelazwa Hospitali ya Mission Ikonda wanaendelea vizuri kwa Mujibu wa Mganga mkuu Wilaya ya Makete Daktari Gaspa Kimaro

Picha na Edwin Moshi

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com