METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, January 4, 2018

MD KAYOMBO AAHIDI MWAKA 2018 MANISPAA YA UBUNGO KILA JAMBO "MCHAKAMCHAKA"

Na Bonwel Kapinga, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John L.Kayombo Amekaririwa akisema kuwa amewaelekeza wakuu wa idara na vitengo kuongeza nguvu katika uwajibikaji na kuwa na viwango vya utendaji katika mwaka 2018.

Mkurugenzi Kayombo amebainisha hayo leo Januari 4, 2018 wakati akizungumza na Waganga Wafawidhi wa Hospitali, CHMT, zahanati na vituo vya afya 18 vinavyotoa huduma katika Manispaa hiyo.

Alisema kuwa Manispaa ya Ubungo imepokea kiasi cha fedha za Basket Fund Tsh 331,886,500.00 na fedha zote hizo zimeingizwa katika akaunti za Benki ya NMB za vituo vya afya, Zahanati na CHMT 18.

Alisema kiasi cha Shilingi 49,782,900 kimeingizwa CHMT, Zahanati Goba Shilingi 14,769,900 , Zahanati Kibamba shilingi 7,753,600 , Zahanati ya kibwegele 7,753,600 , Zahanati kiluvya 7,753,600 , Kituo cha Afya Kimara 29,501,000 , Zahanati ya Kisopya 7,753,600 ,  zahanati ya Kwembe 7,753,600 , Zahanati ya kwembe kati 10,501,000 , na Zahanati ya Mabibo 7,753,600.

Zingine ni Zahanati ya Makuburi 7,753,600 Kituo cha Afya Makurumla 29,501,000 , Zahanati ya Manzese 7,753,600 , Zahanati ya Mavurunza 7,753,600 , Kituo cha afya Mbezi 29,501,000 , Zahanati Msewe 7,753,600 , Zahanati Msumi 7,753,600 , na shilingi 82,971,600 zimeingizwa katika akaunti ya Hospitali ya Sinza.

"Nafahamu kila kiasi cha pesa katika Hospitali, kituo cha Afya, CHMT na Zahanati mlizopewa na maelekezo ya matumizi yameanishwa kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu kanuni na sheria kama zinavyoelekeza na nitafuatilia kwelikweli pesa hizo na matumizi yake alisema" Alikaririwa Mkurugenzi Kayombo

MD Kayombo aliwataka waganga wote wafawidhi kufanya kazi kwa weledi katika vituo vyao vya kazi ili kuendana na kasi ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli huku akiahidi kutembelea vituo vyote wakati wowote iwe usiku au mchana.

Aidha, Mkurugenzi Kayombo alisikiliza baadhi ya changamoto zinazowakabili waganga wafawidhi hao katika Hospitali, vituo vya Afya, CHMT na Zahanati zilizopo katika Manispaa ya Ubungo na kuhaidi kuzitatu ili waweze kufanya kazi vizuri na kwa weledi.

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com