Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara,Mhandisi Stella Manyanya,akiwasili katika Ofisi za wizara hiyo
zilizopo maeneo ya Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma leo.
Waziri wa
Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akisalimiana na Naibu Waziri
wa Viwanda na Biashara,Mhandisi Stella Manyanya,mara baada ya kuripoti
katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo maeneo ya Mtumba nje kidogo ya jiji
la Dodoma akichukua nafasi ya aliyekuwa waziri Joseph Kakunda ambaye
uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akikumbatiana na aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Mhe. Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli kabla ya kukabidhi ofisi kwa Waziri huyo mapema leo jijini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akisalimiana
na watumishi wa wizara yake mara baada ya kuwasili kwa mara ya kwanza
katika Ofisi yake tangu ateuliwe na Rais Magufuli kuchukua nafasi ya
aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli leo amekabidhi ofisi hiyo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akiwa
katika ofisi yake mpya akisaini vitabu mara baada ya kuwasili kwa mara
ya kwanza tangu ateuliwe na Rais Magufuli kuchukua nafasi ya aliyekuwa
waziri Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk.
Magufuli leo amekabidhi rasmi ofisi hiyo.
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara
Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli
akitoa taarifa kabla ya kumkabidhi Ofisi Waziri Mpya Mhe.Innocent Bashungwa tukio hilo limefanyika katika Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akisikiliza
hotuba ya aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Joseph Kakunda
ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli (hayupo pichani)
wakati akitoa taarifa kabla ya kumkabidhi Ofisi tukio hilo limefanyika katika Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akikabidhiwa
rasmi Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Joseph
Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli hafla hiyo
imefanyika katika Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma leo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akiagana
na aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Joseph Kakunda ambaye
uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli mara baada ya kumkabidhi
Ofisi mapema leo hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za wizara hiyo
zilizopo Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma leo.
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara
Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk.
Magufuli,akiagana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhandisi Stella
Manyanya,mara baada ya kukabidhi Ofisi kwa Waziri Mpya Mhe.Innocent Bashungwa leo jijini Dodoma
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akiwa
katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa Wizara hiyo na aliyekuwa
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli,mara baada ya kumkabidhi Ofisi mapema
leo hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara,Mhandisi Stella Manyanya,akizungumza na watumishi wa wizara
hiyo kabla ya kumkaribisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa.
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara
Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk.
Magufuli,akisisitiza jambo kwa watumishi wa wizara hiyo wakati akitoa
neno la kuwaaga na kumkaribisha Waziri Mpya Mhe.Innocent
Bashungwa mara baada ya kumkabidhi Ofisi hafla hiyo imefanyika katika
Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Waziri wa
Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akizungumza na watumishi wa
Wizara hiyo mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa
Viwanda na Biashara Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa
na Rais Dk. Magufuli,hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi
za Wizara zilizopo Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Waziri wa
Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akisisitiza jambo kwa
watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa
rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Joseph
Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli,hafla ya
makabidhiano hayo imefanyika katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba nje
kidogo ya jiji la Dodoma.
Picha na Alex Mathias
………………..
Na.Alex Mathias,Dodoma
Wizara ya Viwanda na Biashara imesema
kuwa kamwe haiwezi kushindwa katika utendajikazi huku ikitoa mambo
muhimu kwa watumishi wake wanapaswa kuyazingatia katika kutimiza azma ya
Rais Dk. John Magufuli, kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa,wakati akiongea na
watumishi wa wizara hiyo baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri
wa Viwanda na Biashara, Josephat Kakunda, ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli.
“Siku zote siamini katika kushindwa na falsafa hiyo lazima ishuke kwa watumishi.”amesisitiza Mhe.Bashungwa
Bashungwa amesema kuwa wizara hiyo ni
muhimu katika kufikia azma ya kuifanya Tanzania kuwa taifa lenye uchumi
wa kati ambao unatokana na maendeleo ya viwanda.
Aidha Waziri Bashungwa ameyataja mambo
matano ambayo ataanza kuyatilia mkazo na kuwataka wafanyakazi
kushirikiana kutimiza majukumu ya kuwatumikiwa Watanzania.
“Kwanza lazima tutumie fursa ya
miundombinu iliyopo katika kuwezesha maendeleo ya viwanda. Rais ametoa
mabilioni ya fedha kujenga reli, bwawa la kuzalisha umeme, barabara,
umeme na mawasiliano.
Hatua ya pili amesema kuwa ni kufanya utafiti utakaobaini mahitaji ya wakulima hususan katika kupata nyenzo za kilimo.
“Katika hili, TIRDO, CARMATEC na SIDO
mjiandae, serikali imeweka mipango mingi ya kuongeza uzalishaji kwenye
kilimo, hivyo taasisi hizo zinapaswa kuja na mkakati wa kuwawezesha
wakulima kupata nyenzo za kuboresha thamani kwenye mazao,” amesema
Mhe.Bashungwa
Ametaja hatua ya tatu ni kubainisha ni
kubaini utendajikazi wa viwanda vilivyobinafsishwa na vile ambavyo
havifanyikazi, hatua zipi zinapaswa kuchukuliwa kwa wakati.
Bashungwa amemalizia kwa kutaja hatua ya
nne ni kuwepo ushirikiano baina ya idara za masoko na biashara kwenye
wizara ya viwanda na ile ya kilimo.
Aidha amewaomba watumishi kutekeleza mpango mkakati uliopo ili kuleta matokeo chanya kwa vitendo.
Awali, Joseph Kakunda ambaye alikuwa
waziri wa wizara hiyo, amesema kuwa katika kipindi cha utumishi wake
amejifunza umuhimu wa Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo mara nyingi
watu wamekuwa wakiilaumu na kuisifu.
Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,
Mhandisi Stella Manyanya, amesema kuwa ni muhimu changamoto
zilizobainika kwenye wizara hiyo zikatumika kama njia ya kuelekea
kwenye mafanikio.
Aliwataka watumishi kufanyakazi bila kukata tama kwa kumpa ushirikiano Waziri Bashungwa ili aweze kutimiza majukumu aliyopewa.
0 comments:
Post a Comment