Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana
wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza jambo
mara baada ya kuwasili ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha leo 11 Januari 2018 kwa
ajili ya ziara ya kikazi ya Siku mbili.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana
wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Kheri Denice James akisisitiza jambo
wakati akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Ndg Loota Sanari mara baada ya kuwasili ofisi
ya CCM Mkoa wa Arusha leo 11 Januari 2018 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya Siku
mbili.
Mazungumzo yakiendelea
Na Mathias Canal, Arusha
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)
Taifa Ndg Kheri Denice James amewasili Mkoa Arusha Jana 10 Januari 2018 kwa
ajili ya ziara ya kikazi ya Siku mbili.
Kheri ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM anatarajiwa
kuongoza kampeni za kumnadi Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi
Jimbo la Longido katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika kesho kutwa 13
Januari 2018.
Pamoja na Mkutano wa hadhara lakini pia atazungumza na wanachama
wa CCM katika Mkutano wa ndani utakaofanyika katika Kijiji na Kata ya Mudarara,
Wilayani Longido.
Chama Cha Mapinduzi CCM kinaingia kwenye uchaguzi huu huku
kikiwa na kumbukumbu ya rekodi nzuri ya ushindi wa kishindo uliofanyika katika
uchaguzi mdogo uliofanyika nchini kwa kuhusisha vyama vyote ambapo CCM
ilishinda kwa jumla ya kata 42 kati ya 43.
Uchaguzi wa Ubunge Jimbo La Longido unafanyika kutokana na
mahakama ya Rufaa nchini kutengua ushindi wa aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo
Onesmo Ole Nangole kutokana na ukiukwaji wa demokrasia katika uchaguzi Mkuu
mwaka 2015.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment