METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, December 22, 2017

ZOEZI LA KUPIGA CHAPA MIFUGO LAZIDI KUNOGA WILANI SAME

Na Mawandishi Wetu, Kilimanjaro

Imekuwa ni safari ndefu iliyoanza na uhamasishaji wa viongozi wa wafugaji - Wazee, chama cha wafugaji, Aleigwanani na viongozi wa vitongoji, vijiji,  kata na baadaye wananchi wote katika zoezi elekezi la serikali kwa wafugaji Wote nchini kupiga chapa mifugo yao kwa ajili ya utambuzi.

Hamasa hii imepelekea wafugaji kujitokeza kwa wingi katika  zoezi la kugonga mihuri kwa mifugo. 

Timu ya Mkuu wa Mkoa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Maafisa Tarafa na wataalamu wa mifugo wamehusika na zoezi linaloendelea ambapo hadi sasa ng'ombe 31950 wamekwisha gongwa mihuri.

Mhe Rosemary Senyamule ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Same amezungumzia jukumu hill na kusema kuwa zoezi hili litaenda na mpango wa taifa, Mkoa na Wilaya ambapo wanategemea kutenga eneo la Ranchi kwa wafugaji, kujenga mabwawa ya maji na baadaye kuhamasisha uwekezaji wa viwanda vya mazao ya mifugo. 

Lengo ni kuhakikisha wafugaji wanapata haki sawa na makundi mengine ya jamii. 

Mhe Senyamule aliagiza idara ya ardhi kuweka alama maeneo yote yaliyoainishwa kwa ajili ya wafugaji ili kuondoa migogoro isiyo na lazima. Pia kutekeleza maagizo ya viongozi ya kuanzisha SACCOS/ Ushirika wa wafugaji. 

Alitoa wito kwa wafugaji kuendelea kupeleka mifugo yao kwa wingi ili Wilaya ijue idadi kamili ya mifugo iliyopo na kupanga mipango inayoendana nayo. 

Kauli mbiu iliyotumika katika zoezi hilo ni

"Mifugo yetu, Utajiri Wetu"

MWISHO.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com