Judith Ferdinand, Mwanza
Wadau wa elimu mkoani Mwanza wametakiwa kuhakikisha vituo vya elimu vinasajiliwa ili kuleta chachu ya kimabadilikio katika sekta hiyo.
Mkufunzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Said Kayege aliyasema hayo juzi wakati akichangia mada kwenye kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Kayege alisema ili kuwa na elimu bora, wadau wana wajibu wa kuthibiti ubora na kuhakikisha vituo hivyo vinasajiliwa kabla ya kuanza kutoa elimu na ambavyo havizingatii taratibu hizovichukuliwe hatua stahiki za kisheria ikiwemo kuvifunga.
Hata hivyo aliwashauri wadau wa elimu kupaza sauti zaidi ili kusaidia kuboresha mazingira ya kusomea na pia kusaidia mitihani ya majaribio (QT) kuwa na tija ikiwemo kufanyika kwa siku mbili badala ya siku moja kama ilivyo sasa.
“Kwa sasa dhana ya mitihani hiyo inapotea baada ya serikali kushindwa kutoa utaratibu nzuri ambapo imebaki kusahili na kuratibu vituo vya masomo ya sekondari pekee.” Alisema.
Kayege aliiomba serikali kutizama upya suala la mitihani hiyo na kutoa utaratibu wa kufanya mitihani ya QT kama ya kidato cha pili kwa zaidi ya siku moja na kila somo ni vyema likafanyika peke yake badala ya kuchanganya masomo yote kwenye mtihani mmoja.
Vilevile alisema watahiniwa wa kujitegemea wanaofanya mitihani ya kidato cha nne hutozwa kiasi kikubwa cha fedha kwa ajli ya kituo cha mitihani hali ambayo huchangia kukwamisha harakati za watanzania kujiendeleza kielimu.
0 comments:
Post a Comment