Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WOTESAWA, Angel Benedicto amesema kasi ya watoto kuajiriwa kufanya kazi za nyumbani inazidi kuongezeka Jijini Mwanza.
Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na shirika la WOTESAWA katika Kata nne za Manispaa ya Ilemela ambazo ni Kitangiri, Kawekamo, Nyasaka na Kiseke umebaini watoto zaidi ya 400 walioajiriwa kufanya kasi za nyumbani.
Hata hivyo shirika hilo kupitia mradi wake wa Paza Sauti ya Mfanyakazi wa Nyumbani unaofadhiliwa na Shirika la The Voice kupitia serikali ya Uholanzi, limeanza kutoa elimu kwa viongozi wa serikali za mitaa wakiwemo Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Mitaa, waajiriwa wa kazi za nyumbani pamoja na waajiri wao ili kupambana na hali hiyo katika Kata tajwa hapo juu ambazo zinanufaika na mradi huo.
Soma BMG Habari, Pamoja Daima kuhusu mradi huo.
Je nini kifanyike kuzuia ajira kwa watoto ili kuwawezesha kupata Haki zao za msingi ikiwemo Elimu? #WoteSawa #PamojaDaimaBMG Wasilisha maoni yako hapa na shirika la WOTESAWA litayafanyia kazi. Ama piga 0800 7100 60
0 comments:
Post a Comment