Naibu
Waziri OR TAMISEMI Mhe. Joseph G.Kakunda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya Viongozi wa Mkoa wa Arusha, wilaya ya Longido, Ofisi ya Rais TAMISEMI na
Haki kazi Catalyst wa mjini Arusha
Naibu
Waziri OR TAMISEMI Mhe. Joseph G.Kakunda akitoa maelekezo kwa watendaji wa maji
katika mradi wa maji wilayani Longido
Serikali imewaagiza
Wahandisi wa maji kuhakikisha wanasimamia miradi ya sekta ya maji nchini
inayozingatia thamani ya shilingi na yenye kuleta tija kwa Watanzania.
Akiongea katika ziara yake
mkoani Arusha katika wilaya ya Longido Mhe. Joseph George Kakunda, Naibu Waziri
Ofisi ya Rais TAMISEMI, amesema kumekuwepo na ufujaji wa fedha za katika Miradi
ya maji nchini na mara nyingi imekuwa sio endelevu na yenye kuleta hasara kubwa
kwa Taifa.
“Wahandisi hakikisheni
mnasimamia utekelezaji wa miradi ya maji kwa thamani ya shilingi, wale wote
wanaojenga miradi hiyo muwasimamie vizuri, fedha tunazozikopa hakikisheni
mnazitumia vizuri, acheni kupokea rushwa, nataka kuona Wahandisi wanajenga
mradi kwa maslai ya watu wa Longido ili kuondoa kero za maji, zingatieni
taratibu, kanuni na sheria ili tupate tunachostahili”
Mhe. Kakunda amewataka
Watendaji na Wahandisi kufanya mapitio ya miradi ya maji nchini ili kuona
miradi iliyotekelezwa kwa halali na pia ili iliyotekelezwa kwa wizi ionekane.
“haiwezekani tangu tuanzishe Programu ya Maji Vijijini tumekwisha tumia zaidi
ya shilingi trilioni 1.6lakini bado kila sehemu kuna shida ya majikwa nini kila
mradi una maisha yake kama miaka 10, 15, 20, 25 hili haliwezekani, hatuwezi
kwenda namna hiyo, mimi nitapendekekeza tufanya mapitio ya miradi yote ya maji
iliyojengwa hasa kuanzia mwaka 2008. Kwanini watu wa kawaida wanajenga mradi
mkubwa kutoka kwenye chanzo hadi hapa”
Akiwa kijijini Elondeka,
Mhe. Kakunda amepongeza hatua zilizofikiwa za Mradi wa maji unaotekelezwa na
Mradi wa Tabia nchi (DCFP)ambao umegharimu kidogo cha fedha shilingi milioni 36
na kushauri wananchi kuulinda siku zote. Pia alikagua mradi wa maji
unaotekelezwa na Halmashauri ya wilaya Longido ambao bado haujakamilika.
Akisoma taarifa ya mradi
mbelel ya Mheshimiwa Naibu Waziri Kakunda, Mtesigwa Missana ambaye ni Afisa
Tarafa Longido amesema kuongezeka kwa kutotabilika kwa tabia ya hali ya hewa
yanazidisha changamoto kama vile kubadilisha mtindo wa maisha ya wananchi.
Aidha, Mhe. Kakunda amewaasa wananchi kuulinda
mradi wao waliouchagua wenyewe, “toeni ushirikiano kwa mradi huu kwa sababu
mmeuchagua wenyewe, lindeni sana mradi huu ili uweze kuhudumia ninyi wenyewe na
mifugo, mradi huu una faida kwenu ninyi, mifugo na wanyama wa porini”
Wananchi walibuni Mradi wa
tanki la maji lenye ujazo wa mita 50,000 unaotekelezwa na Mkandarasi
J.J.Gwakisa ambao upo katika hatua za mwishoni. Mradi wa huo wa maji unaopata
maji toka katika bomba lililotoka kwenye chanzo naotarajiwa kuhudumia watu
4,814 kwa mujibu wa takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012
Kwa upande wake Mkuu wa
Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Njungolo amesema wilaya ya Longido inakabiliwa na
changamoto ya kuwa na watumishi wengi wanaokaimu na kufanya maamuzi yao kuwa
sio ya kuridhisha na pia sekta ya afya imekumbwa na uhaba mkubwa wa watumishi
na kuathiri kabisa utolewaji wa huduma ya afya wilayani humo kwani zaidi ya
asilimia 15 ya watumishi wa sekta hiyo waliondolewa katika zoezi la vyeti
bandia.
Mheshimiwa Kakunda
anaendelea na ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha
kujionea hali ya utendaji na kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo shule, miradi
ya maendeleo na miradi ya tabianchi Mkoani Arusha.
0 comments:
Post a Comment