Serikali mkoani Geita imejipanga kutatua kero ya maji kwa
wananchi inayowakabili wananchi kwa muda mrefu.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ametoa kauli
hiyo alipotembelea miradi ya uzalishaji wa maji inayosimamiwa na Mamlaka ya
maji safi na usafi wa mazingira jinni Geita, GEUWASA.
Alisema serikali imedhamiria kuona mji wa Geita unakuwa na
maji ya kutosha ambapo kwa sasa kuna tanki lenye Mita za ujazo elfu moja na mia
mbili na kwamba zipo jitihada za kuweka
pampu itakayosaidia kuongeza maji kwenye tanki hilo ili kuweza kuongeza zaidi
uzalishaji wa maji kwa maeneo ya mji huo.
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshugulikia
masuala ya Bonde la Ziwa Victoria Dr Ali Said Matano alisema mji wa Geita
utanufaika na awamu ya tatu ya mradi wa maji kutoka Ziwa hilo kwa ufadhili wa
Benki ya Afrika.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
mjini Geita, GEUWASA Bw Joseph Mwita amesema mahitaji ya maji mjini Geita ni
Mita za ujazo 15 160 na kwamba maji
yanayozalishwa ni Mita za ujazo kati ya
3 500 hadi 4000.
0 comments:
Post a Comment