METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, December 28, 2017

MSIWACHEKEE WANAOVUNJA HESHIMA KWA VIONGOZI WETU: KHERI JAMES

Mwenyekiti mpya wa Umoja wa vijana Chama cha mapinduzi (UVCCM) Kheri James amewahutubia vijana mbalimbali visiwan Zanzibar na kuwasihi kutowachekea wanaovunja heshima kwa viongozi.
Kheri James ameyasema hayo alipowasili katika ukumbi wa Gymkhana visiwan humo 27December, 2017 alasiri na kupokelewa kwa mapokezi mazito.
Kheri alipokelewa na Afisa mkuu Zanzibar na Juma Sadala Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar aliyeambatana na Makamu mwenyekiti UVCCM Taifa Thabia Mwita, Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka, Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Morogoro Ramadhani Kimwaga, Mwenyekiti Kanda Maalumu ya DSM UVCCM Musa kilakala, Joan Katarahiya Mjumbe Baraza kuu Taifa Viti 5 Tanzania Bara, Hadija Keisha MNEC, Mohamed.
Pia Abdallah kaimu katibu wa idara ya organization Uhusiano wa kimataifa na baadhi ya Maafisa makao makuu. Mwenyekiti Kheri alipata Burudani kutoka kikundi cha Zanzibar Big Star, vijana wa wilaya Dancers pia alipokea zawadi mbalimbali kutoka mikoa yote ya Zanzibar
“Ni marufuku kutukana na kuvunja heshima za viongozi wa nchi hii. Ni marufuku kwa UVCCM kulinda Watu wanaotukana viongozi, hata awe Mwana CCM hatutakubali hilo.” alisema Kheri.
Kheri alisisitiza Vijana kubadilika na kuwa imara, madhubuti wenye ujasiri wa kujiongoza pasipo kunyenyekea mtu.
Kheri alisema: “Zama zangu sihitaji viongozi biskuti bali nahitaji Vijana imara shupavu, wanaojua majukumu yao na wasioyumbishwa. Habari ya Vijana kulamba miguu viongozi siitaki ndani ya utawala wangu”.
Kheri ambaye ameanza uongozi wake kwa kuanza zoezi la uhakiki wa Mali za jumuiya ameibuka na tume nyingine ya uhakiki wa Watumishi wa UVCCM.Kheri alibainisha: “Tunakwenda kufanya uhakiki wa Wafanyakazi hewa ndani ya jumuiya ya Vijana ambao wanapewa mishahara hewa ama wanapata mishahara lakini hawafanyi kazi zao vyema”.
“Mariam Chaurembo na Sophia Kizigo wanatoka tume ya uhakiki wa Mali za jumuiya na kuwa Wajumbe wa awali wa tume ya kuhakiki Wafanyakazi hewa” alisisitiza Kheri James
Kheri akuacha kukazia juu ya suala la uhakiki wa Mali za jumuiya kuwa si hiari na asiyeweza atupishe.
Kheri alibainisha: “Nahitaji maagizo yangu ya uhakiki wa Mali za Jumuiya ufanyike. Viongozi wa jumuiya ngazi zote tambueni majukumu yenu na asiyeweza atupishe”.
Pia alieleza sababu za kutokuteua Wajumbe toka Zanzibar kwenye tume ya uhakiki wa Mali za jumuiya, kuwapa nafasi kubwa ya kujihakiki wenyewe.
“Kwenye tume niliyounda ya kuchunguza Mali za jumuiya sikuweka hata Mzanzibar mmoja. Nataka Mali na rasilimali za Zanzibar zihakikiwe na Wazanzibar wenyewe” alisema Kheri James.
Naye Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka H. Shaka alisisitiza ushirikiano wa kutosha kati yake na Mwenyekiti Kheri James kwa maslahi mapana ya UVCCM.
“Mwenyekiti Kheri James tupo tayari kushirikiana nawe daima, tupo pamoja sote kuhakikisha tunaijenga jumuiya ya UVCCM” alisema Shaka.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com