METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, December 1, 2017

Mkuu wa Chuo cha Watoa Tiba kwa Vitendo Tanzania atunukiwa Tuzo ya Heshima

Rais wa Chama cha Watoa Tiba Tanzania TOTA, Bi.Neophita Lukiringi akizungumza kwenye kongamano la chama hicho jijini Mwanza.
Mkuu wa Chuo cha Watoa Tiba kwa Vitendo nchini (The School of Ocupational Theraphy KCMC) kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro, Bi.Sarah Mkenda ametunukiwa Tuzo heshima ili kutambua mchango wake wa kuendeleza sekta hiyo.
Awali tuzo hiyo ilikuwa ikishikiliwa na mwasisi wa chuo hicho, Bi.Herma Grossmann tangu mwaka 2004 hadi mwaka huu.
Aidha Bi.Grossman pia amemkabidhi Bi.Mkenda Medali ya Shaba aliyotunukiwa na chama cha Watoa Tiba kwa Vitendo Duniani (World Federation of Occupational Therapists) ambapo naye atamkabidhi mtoa tiba kwa vitendo nchini atakayetoa mchango mkubwa katika sekta hiyo.
Mkenda amekabidhiwa Tuzo na Medali hiyo hii leo Jijini Mwanza kwenye kilele cha Kongamano la Chama cha Watoa Tiba kwa Vitendo Tanzania TOTA, lililoanza juzi Novemba 29 likitanguliwa na huduma ya ushauri na tiba kwa vitendo kwa wananchi bure.
Watoa tiba kwa vitendo ni wataalamu wa afya wanaotoa ushauri na matibabu ya viungo kwa walemavu kwa kutumia vitendo/ mazoezi ambapo watu wenye ulemavu hususani wenye ulemavu wa viungo na akili wakipata tiba hiyo mapema hupata ahueni na uwezo wa kuendelea na shughuli zao za kila siku kama kawaida.
Wajumbe wa kongamano hilo wakimsikiliza Rais wa TOTA.
Mwasisi wa TOTA na chuo cha watoa tiba nchini Bi.Herma Grossmann (kushoto), akimkabidhi Bi.Sarah Mkenda (kulia) nishani/cheti cha utambuzi kwenye sekta ya utoaji tiba kwa vitendo nchini.



Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com