METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, December 15, 2017

MKANDARASI WA MRADI WA MAJI BUYAGU KIKAANGONI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujeniz wa barabara ya lami inayojengwa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini(Tarura) mjini Sengerema.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo amemuagiza mkandarasi wa mradi wa maji Buyagu kukamilisha mradi huo kabla mwishoni mwa mwezi Februari 2018 la sivyo ataingia matatani.

Jafo alionyesha kukerwa kutokana na utendaji duni ulionyeshwa na mkandarasi huyo D4N Co. Ltd. 

Mradi huo ulianza mwaka 2014 na unagharimu shilingi za kitanzania bilioni 1.7

Katika ziara hiyo wilayani sengerema Jafo amewasihi watendaji kujituma wakati wanatimiza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.

Waziri Jafo alifanikiwa kutembelea mradi mwingine wa ujenzi wa barabara ya lami na amemuagiza meneja wa Tarura Halmashauri ya Sengerema kusimamia ubora wa barabara zinazojengwa katika Halmashauri hiyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com