METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, December 28, 2017

MAVUNDE AWATAKA POLISI JAMII KUUNDA VIKUNDI VYA UZALISHAJI MALI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

 Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony Mavunde akifunga mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma.
 Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony Mavunde akiwa na Kamanda wa polisi Dodoma Gilles Murotop wakikagua gwaride katika ufungaji wa mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma.
 Vikundi vya Ulinzi shirikishi
 Vikundi vya Ulinzi shirikishi
Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony Mavunde akimvisha utambulisho mmoja wa washiriki wa mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma

Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony Mavunde amewataka Vijana ambao wanashiriki katika mafunzo ya Ulinzi shirikishi kupitia Polisi Jamii kuunda vikundi vya uzalishaji mali ili kujikwamua kiuchumi na kuongeza kipato.

Mavunde ameyasema hayo leo wakati akifunga mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma.

“Pamoja na jukumu kubwa mlilonalo na ulinzi na usalama wa raia na mali zao,lakini pia mhakikishe mnatumia mkusanyiko wenu kuunda vikundi vya uzalishaji mali ili kujiongezea kipato na kutengeneza nafasi za Ajira zaidi,”amesema

Mavunde amewataka vijana hao kuyatumia vyema mafunzo waliyopata kwa kuwa waadlifu,waaminifu na wazalendo kwa Taifa lao na kusimama mstari wa mbele kuhakikisha Taifa hili linaendelea kuwa na AMANI na UTULIVU.

Naye, Kamanda wa Mkoa wa  Polisi wa Dodoma,SACP  Gilles Muroto amewataka Vijana zaidi kujitokeza katika Ulinzi shirikishi ili kuimarisha usalama na amani katika mkoa wa Dodoma.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com