METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, December 19, 2017

Mambo ni Moto Mjini Dodoma kwenye Mkutano Mkuu wa CCM

 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akifungua Mkutano Mkuu wa tisa wa CCM, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma, leo. Pamoja na mambo mengine kuhusu mageuzi ndani ya Chama, uadilifu na usimamizi wa mali za Chama ili Chama kisitegemee wafadhili wakiwemo matajiri wachache, amemtaka Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana kuendelea kumsaidia katika nafasi hiyo ya Katibu Mkuu katika kipindi kingine cha miaka mitano.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsalimia Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, alipokuwa akisalimia mabalozi kutoka nchi mbalimbali ambao wamehudhuria Mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo wakikagua mazingira ya nje ya ukumbi kabla ya mkutano huo mkuu kuanza.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akiandaa mazingira ya kuchangamsha ukumbi kabla ya mkutano huo kuanza. Kushoto ni katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
 Wanakwaya wa TOT wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha ukumbini Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk John Magufuli.
 Wajumbe wakijimwayamwaya ukumbini kushangilia wakati Mwenyekiti wa CCM Taifa, akiingia ukumbini.
 Mwimbaji wa TOT akiimba wimbo wa kuhamasisha mapokezi ya Mwenyekiti ukumbini
 Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Jakaya Kikwete na Mwenyekiti mstaafu wa CCM Ali Hassan Mwinyi wakimsubiri Mwenyekiti Kuingia Ukumbini. Mzee Mwinyi akisoma toleo maalum la gazeti la Uhuru wakati akisubiri.
 Viongozi waliotangulia meza kuu wakisimama kumlaki Mwenyekiti wa CCM rais Dk John Magufuli wakati akiingia ukumbini.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli akisalimia viongozi mbalimbali baada ya kuingia ukumbini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli akiwa tayari ukumbini. Wengine kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa CCM Rais wa Zanzibar Dk. Shein, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM-bara Philip Mangula na Mwenyekiti Mstaaafu wa CCM Benjamin Mkapa
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Maguduli akijadili jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana baada ya kuketi ukumbini.
 Waimbaji wa TOT wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya Mkutano kuanza.
 Wajumbe wakiwa wamesimama kuimba wimo wa Taifa.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli na viongozi wengine meza kuu wakiimba wimbo wa Taifa huku wamesimama kwa ukakamavu.
 Viongozi wakiw wameketi baada ya kuimba wimbo wa taifa.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiondoka meza kuu kwa ukakamavu kwenda kufuatilia jambo.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti kufungua Mkutano huo.
 Wapicha picha wakifuatilia matukio
 Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Mama Maria Nyerere akiwa na Mama Salma Kikwete kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya wageni waalikwa na wajumbea wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Magufuli (kulia)akifungua mkutano huo mkuu.
 Wajumbe wakishangilia baada ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Magufuli kumtaka Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuendelea kumsaidia katika nafasi hiyo ya Ukatibu Mkuu kwa miaka mingine mitano.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akionekana kutafakari baada ya kauli ya Mwenyekiti wa CCM Dk Magufuli  kumhitaji tena.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiinuka kuonyesha ishara ya kukubali makakwa ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Magufuli. Kulia ni Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Zanzibar Dk Amani Abeid Karume na Mzee Mkapa ambaye anacheka kuonyesha kuunga mkono.
 Baadhi ya waliohamia CCM kutoka vyama vya upinzani wakisimama baada ya kutmbulishwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Magufuli kwenye mkutano huo.
Jioni hii Dkt.John Pombe Magufuli amechaguliwa kuendelea kuhudumu nafasi yake ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM. Pia viongozi wengine tayari wametangazwa kwenye mkutano huo.
Picha na Bashir Nkoromo, Dodoma.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com