METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, July 17, 2021

NAIBU WAZIRI BYABATO ATEMBELEA KITUO CHA KUZALISHA UMEME WA JUA KIGOMA

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za mwanga wa jua cha Nextgen Solawazi LTD Lakhan Gupta, alipotembelea Kituo hicho kilichopo Mkoani Kigoma.

 

Paneli zinatumika kubadilisha mwanga wa jua kwenda kwenye umeme.

 Na Dorina Makaya – Kigoma.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato amesema, Wizara ya Nishati itashirikiana na kumsimamia mwekezaji wa kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za mwanga wa jua cha Nextgen Solawazi LTD kilichopo Mkoani Kigoma ili kuhakikisha anafikisha uzalishaji wa 5MW kama ilivyokubalika kwenye mkataba uliosainiwa.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato ameyasema hayo tarehe 16 Julai, 2021 alipotembelea kituo hicho  cha kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za mwanga wa jua cha Nextgen Solawazi LTD

Kituo hicho kina uwezo wa kuzalisha umeme 4MW

Hivi sasa Kituo hicho kinazalisha umeme 1.8 MW. zinazopelekwa kwenye kituo cha umeme cha TANESCO mkoa wa Kigoma.

Naibu Waziri wa Nishati amempongeza mmikiki wa kituo hicho kwa hatua aliyofikia na kuahidi kuwa Wizara ya Nishati itashirikiana na mwekezaji huyo ili kuhakikisha anafikisha uzalishaji wa 5MW kama ilivyokubalika kwenye mkataba uliosainiwa.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Byabato aliambatana na  Kaimu Mkurugenzi wa Umeme na Nishati Jadidifu Edward Ishengoma, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji Umeme TANESCO, Mha. Isaac Chanji, Mkurugenzi Mkuu REA Mha. Amos Maganga, Meneja Mwandamizi Kanda ya Magharibi Mha. Sana Idindili, Meneja wa TANESCO mkoa wa Kigoma Jaffari Mpina, na baadhi ya watumishi wa TANESCO na REA.

Tanzania ni nchi mojawapo inayoweza kunufaika na vituo vya kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za mwanga wa jua kwa sababu inapata mwanga wa jua kwa kipindi kirefu katika mwaka.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com