WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo ameonyeshwa kukerwa na uchafu uliokithiri katika soko la Mabibo lililopo wilayani Ubungo jijini Dar as salaam.
Soko hilo maarufu kwa jina la Mabibo-mahakama ya ndizi limetapakaa maji machafu na madibwi yanayotoa harufu mbaya.
Jafo amesema uchafu huo ni hatari sana kwa afya ya wananchi kwani wanaweza kupata magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa kipindupindu.
Kutokana na hali hiyo, Jafo ameielekeza manispaa ya ubungo kufanya marekebisho ya haraka ikiwa ni pamoja na kufukia madimbwi na kusambaza kokoto sokoni hapo pamoja na kuweka mfereji wa kupitishia maji.
Pia Jafo amewataka watendaji wa soko hilo kusimamia mapato ipasavyo kutokana na ukusanyaji mapato kuwa hauridhishi.
Amesema wastani wa sh.milioni 90 kwa mwezi zinakusanywa ikilinganishwa na biashara kubwa ya ndizi na viazi inayofanywa sokoni hapo.
0 comments:
Post a Comment