Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani
Jafo amewasisitiza viongozi wa mkoa wa Kagera kutokubadilisha malengo ya shule
ya Ihungo kwa kuigeuza kuwa chuo kikuu baada ya kukamilika kwa ujenzi.
Jafo ameyasema hayo alipokuwa akikagua
maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo inayojengwa upya baada ya hapo awali kukumbwa
na tetemeko la ardhi.
Shule ya Ihungo inajengwa kisasa na
itakapokamilika itakuwa shule ya kipekee kwa kuwa na miundombinu ya kisasa hapa
nchini.
Amesema Majengo ya shule hiyo kwasasa yanaweza
kuwatamanisha baadhi ya viongozi kutaka kubadilisha shule hiyo hapo baadae kuwa
chuo kikuu kitu ambacho amezuia jambo hilo.
Amesema amezuia ili vijana wa kidato cha tano
na sita ili waweze kupata nafasi kusoma katika shule hiyo yenye mazingira
mazuri.
Baada ya ukaguzi wa shule hiyo,Waziri Jafo
alielekea na ukaguzi wa shule nyingine ya Nyakato inayojengwa na Suma JKT na
kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi.
0 comments:
Post a Comment