Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo ameagiza kufanyika uchunguzi wa haraka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya morogoro Vijijini Sudi Mussa Mpiri kutokana na utendaji wake kutoridhisha ikiwemo kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo.
Pia ameshindwa kutoa ufafanuzi wa fedha zilizopokelewa na Halmashauri hiyo kiasi cha sh.milioni 1.6 ya mapato ya ndani kutoka kampuni ya Dimond ambapo matumizi ya fedha hiyo zaidi ya asilimia 90 hayafahamiki kilichofanyika.
Kadhalika, Mkurugenzi huyo anadaiwa kuwa na mahusiano mabovu kati yake na watumishi wa Halmashauri hiyo.
Jafo alitoa agizo hilo akiwa Kijijini Mvuha kwenye makao makuu ya Halmashauri ya morogoro vijijini.
Kutokana na hali hiyo,Jafo ameagiza kitengo cha uchunguzi na ufuatiliaji kilichopo Ofisi ya Rais TAMISEMI kufika haraka kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini mwenendo wa mkurugenzi huyo kwa lengo la kuchukua hatua stahiki endapo itabainika kuna ufisadi na mapungufu ya kiuongozi kwa mkurugenzi huyo.
Katika hatua nyingine, Waziri Jafo hajarishishwa kabisa na miradi aliyo itembelea wilayani humo kutokana na miradi hiyo imeonyesha wazi kwamba Halmashauri hiyo imefanywa kama shamba la bibi.
0 comments:
Post a Comment