Shughuli
ya kufunga hotel hiyo imefanyika leo Novemba 9 asubuhi saa 12 huku
wateja waliokuwa bado wamelala wakilazimika kuamshwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo, Scholastika Kevela amesema hotel hiyo
inadaiwa kodi ya pango na Ubungo Plaza Sh.5.7 bilioni.
"Tunafunga na kukabidhi kwa mmiliki na shughuli hapa hazitaendelea tena hadi awe amelipa kodi," amesema Kevela
Mmoja
wa wateja, Masoud Masoud akiwa na familia yake amesema''nimetoa hela
nyingi na ilikuwa nikae kama wiki mbili na nimeingia jana, huu ni
usumbufu."
0 comments:
Post a Comment