Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Henry Kinabo(kulia)
akizungumza na waandishi wa habari jana namna ya kujisajili mbio za
Dodoma Marathon zitakazotimua vumbi jumapili ya tarehe 12 mwezi huu,
ambapo utaweza kujisajili kwa Tigopesa kwa namba 0674 444 444 kwa
punguzo la asilimia 10%. Pembeni ni Meneja wa Maendeleo wa Vision
Sports, Raymond Mchani. **** Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya
kidigitali, Tigo Tanzania wakiungana na Vision Sports wametangaza kuanza
kwa usajili wa washiriki katika mbio za Dodoma Marathon. Mji wa Dodoma
utageuzwa kuwa kitivo cha mazoezi na furaha kwa familia nzima tarehe 12
Novemba wakati shindano hilo litakapohitimishwa. Usajili kwa Dar es
Salaam unafanyika katika vituo maalum vya Duka la Tigo Shop lililopo
Mlimani City, Duka la Simply Elegant lililopo Dar Free Market, Ghorofa
ya Chini ya Kibo Complex eneo la Tegeta na Duka la Imalaseko SuperMarket
lilipo eneo la Posta katikati ya jiji. Kwa Dodoma, usajili unafanyika
katika eneo la Dodoma Hotel, Carnival, Cape Town Complex iliyopo Kisasa
na Duka la Tigo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). ‘Wale
watakaojisajili kwa njia ya Tigo Pesa watapata punguzo la bei la
asilimia 10%. Wanaweza kufanya hivyo kwa kutuma kiasi cha shilingi
13,500/- kutoka kwenye simu zao za mkononi kwenda namba ya Tigo Pesa
0674 444 444. Hapo hapo watapokea ujumbe utakaowataarifu kujisajili na
eneo ambalo wanafaa kwenda kuchukua vielelezo vyao vya usajili,’ Meneja
wa Tigo, Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo alisema. Kwa upande
wake,Meneja wa maendeleo wa Vision Sports, Raymond Mchani kwa niaba ya
Ally Nchahaga, Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Sports aliwashauri
washiriki kusoma vigezo na masharti ya ushiriki pamoja na taarifa
nyingine muhimu kutoka kwenye tovuti ya Dodoma Marathon na katika vituo
vya usajili. ‘Pia ni muhimu kwa washiriki kuhudhuria kikao cha maelezo
kuhusu ushiriki na usalama wa washiriki kitakachofanyika kabla ya mbio
kuanza saa kumi na mbili asubuhi, pale katika Uwanja wa Jamhuri, mjini
Dodoma. Tigo inathamini mbio za kilometa 21 za Tigo Dodoma Half
Marathon. Dodoma Marathon pia itahusisha mbio ndefu za kilometa 42,
mashindano ya kilometa 10 pamoja na yale ya kilometa 5 yatakayohusu
wanafamilia na jamii yote kwa ujumla. Zawadi murwa zitatolewa kwa
washiriki ikiwemo vyeti vya ushiriki, medali na zawadi za fedha kwa
washindi wa mbio zote. Wanariadha mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi
wanatarajiwa kushiriki katika mbio hizo. “Tuna furaha kubwa
kudhamini shindano hili ambalo linahamasisha watu kuzingatia afya bora
kwa kushiriki katika michezo, na pia kuinua vipaji katika michezo,”
Henry Kinabo, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini alisema. Kuhusu Tigo:Tigo
Tanzania ni kampuni ya simu inayotoa huduma bora za maisha ya
kidigitali nchini Tanzania. Tigo ilianza kuendesha shughuli zake nchini
Tanzania mwaka 1995.Kupitia huduma zake za kipekee za sauti, ujumbe
mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha kupitia simu za
mikononi, Tigo inaongoza kwa ubunifu wa kidigitali kwa kuwa kampuni ya
kwanza Tanzania kuzindua facebook na smartphone zenye lugha ya
Kiswahili, huduma ya TigoPesa, pamoja na huduma ya kwanza inayowezesha
wateja kufanya miamala ya fedha kupitia simu za mkononi kwenda nje ya
nchi yenye uwezo wa kubadili thamani ya fedha kwa sarafu ya nchi husika
Afrika Mashariki.
Tigo ni kampuni ya simu ya pili kwa ukubwa nchini
na ni kampuni ya simu inayokuwa kwa kasi zaidi nchini kwa kipindi cha
miaka mitatu mfululizo. Kupitia mkakati mkubwa wa kupanua na kuboresha
huduma zake, kati ya mwaka 2015 hadi 2016, Tigo ilizindua mtandao wa 4G
LTE jijini Dar es Salaam na katika miji mingine 22 nchini.
Tigo
inajivunia jumla ya watumiaji milioni 10 wa simu waliosajiliwa, na
imetoa nafasi za ajira za moja kwa moja na zile zisizokuwa na moja kwa
moja kwa Watanzania wapatao 300,000; hii ikiwa ni pamoja na wawakilishi
wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha kupitia simu za
mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.
Tigo ni nembo ya
kibiashara ya Millicom, kampuni ya kimataifa inayoongoza mageuzi ya
maisha ya kidigitali katika nchi 13 duniani. Ikiwa inaendesha shughuli
zake za kibiashara katika bara la Afrika na Amerika ya Kusini, Ofisi kuu
za Millicom zipo Ulaya na Marekani.
Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz
Malunde
0 comments:
Post a Comment