#"Miaka 25 ya uwepo wa vyama vingi vya upizani CCM haikuyumba wala kutetereka, upizani ulianza kwa udhaifu na utamaliza ukiwa dhaifu kwa kuwa hawana mipango wala mikakati ya kuvijenga vyama vyao na kuwa taasisi kamili za kisiasa kama kilivyo Chama Cha Mapinduzi " Shaka
#"Vyama bora vya siasa ni lazima viwe na katiba, miuundo bora ya uongozi na sera zinazojali maslahi ya umma na kutetea wananchi wanyonge na masikini kama kinavyofanya chama cha Mapinduzi kilichotokana na vyama vya vya TANU na ASP" Shaka
#"Mhe Magufuli, mhe Samia, mhe majaliwa, mama Nagu wote waliandaliwa na kupikwa na CCM na leo ni viongozi wanalitumikiaTaifa na Portajia ameandaliwa na amewiva na sasa yuko tayari kuwatumia wana Nangwa mpeni kura kesho" Shaka.
#"Nawapongeza vijana wenzangu kwa kukataa kunasa katika mtego siasa za ghiliba na hadaa za vyama vya upizani ambavyo vilikusudia kuwapotosha vijana kuwapumbaza kifkra na kujaribu kuwaondolea uaminifu utii na uzalendo wa kulitumikia taifa lao" Shaka
#"Nazungumza na watanzania kupitia wananchi wa Nangwa nikiwaeleza kwamba upizani hauwezi kusimama na kukubalika mbele ya watanzania kwa kuwa vyama hivyo vimeundwa na viongozi waliofukuzwa CCM aidha kwa usaliti, ukuwadi wa kisiasa au kushiriki kwao katika vitendo vya rushwa, ubadhirifu wa mali za umma." Shaka
#"Aina ya viongozi kama hawa wakubaliki katika mbele ya watanzania vipi wataungwa mkono na kuwaamini kuwapa kura " Shaka
#"Chama hiki CCM ndicho chama kilichowakomboa watanzania na sehemu kubwa katika bara la Afrika, chama hiki ndicho alichotoka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndicho alichotoka Rais wa kwanza wa Zanzibar na mpigania uhuru wa Afrika hayati Mzee Abeid Amani Karume" Shaka
#"Ndicho chama alichotoka Mzee Rashid Kawawa Simba wa vita, Mzee Thabit Kombo, Mzee Msekwa, hayati Aboud Jumbe Mwinyi na viongozi wengine waadilifu, waaminifu, na wazalendo halisi ambao hawana tuhuma za unyonyaji, dhulma ama kushiriki ufisadi" Shaka
#"Wananchi na wakaazi wa kata ya Nangwa kesho mkimchagua Portajia kuwa diwani wenu mtakuwa hamjapoteza lolote bali mtakuwa mumeendelea kuwaenzi na kuwaheshimu wapigania uhuru wa Taifa letu " Shaka
#"Kwa bahati mbaya hata viongozi wa upizani walioshiriki kuviunda vyama hivyo wamekata tamaa wamevipuuza na wengine wameamua kufanya maamuzi sahihi kurudi CCM" Shaka
#" Rais Magufuli alitembea nchi nzima kunadi ilani ya uchaguzi ambayo sasa tunaitekeleza kwa mafanikio makubwa kwa Jimbo la Hanang anasaidiwa na Mama Merry Nangu mpeni na Portajia waungane watatu kuleta maendeleo endelevu kiuchumi na kijamii Nangwa na Hanang kwa ujumla" Shaka
#"Sifa kubwa ya CCM ni kuandaa viongozi wazuri mama Portajia ana uwezo mkubwa katika kutenda mpeni aje ashirikiane na Mbunge kutatua kero ya maji , Barabara na kukamilisha shule mlizojenga kwa nguvu zenu" Shaka
#"Bahati mbaya kwa miaka 7 mumeteseka na upizani mkombozi wenu ni Portajia wa CCM mchagueni kesho, achaneni na hao matapeli wenzi wa asilimia 5 za vijana na wakinamama ameiba hata calvat zilizotolewa kwa ujenzi wa Barabara na kuenda kuuza" Shaka
0 comments:
Post a Comment