MKUTANO wa Tisa wa Bunge unaendelea leo huku miswada minne
ikitarajiwa kuwasilishwa ukiwemo wa kutungwa Sheria ya kuanzisha Shirika
la Mawasiliano wa Tanzania na kufuta Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Pamoja na mambo mengine, shirika hilo litakuwa na kazi ya kutoa
huduma za kiufundi, ushauri na kihandisi kuhusu Tekonolojia ya
Mawasiliano kwa taasisi za Serikali. Pia kutawasilishwa Muswada wa
kuanzisha Shirika la Wakala wa Meli ambalo litakuwa na jukumu la kutoa
huduma za uwakala wa meli na kudhibiti huduma za usafiri na usalama wa
vyombo vya majini.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Bunge, muswada huo
mawasiliano utawasilishwa kesho. Mbali na kutoa huduma hizo kwa taasisi
za Serikali, pia itatoa huduma kwa mashirika makubwa na madogo,
wajasiriamali wadogo na wa kati na mamlaka nyingine. Muswada wa
kuanzisha Shirika hilo la Mawasiliano Tanzania wa mwaka 2017, unaeleza
Ofisa Mtendaji Mkuu atateuliwa na Rais na wafanyakazi na mali zote za
TTCL zitahamishiwa kwenyeshirika hilo na bila kutozwa kodi.
Vile vile unabainisha kuwa TTCL Pesa itakuwa kampuni tanzu ya shirika
hilo la mawasiliano huku ikiendelea na kazi zake za huduma za kifedha.
Miswada mingine itakayowasilishwa wiki hii kabla ya kuahirishwa kwa
Bunge Ijumaa ni wa Sheria ya Wakala wa Meli Tanzania wa Mwaka 2017.
Mingine ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali
Namba 4 wa Mwaka 2017 na Muswada wa Marekebisho ya Sheria Kudhibiti na
Kupambana na Dawa za Kulevya wa Mwaka 2017. Miswada hiyo itasomwa katika
hatua zote. Katika muswada wa kuanzishwa Wakala wa Meli, majukumu yake
yanatajwa kuwa ni kuhakiki shehena inayoingia na kutoka kupitia bandari
za Tanzania.
Mengine ni uondoshaji shehena za madini, makinikia, nyara za
Serikali, wanyama hai, bidhaa zitokanazo na madini na udhibiti wa watoa
huduma katika sekta ndogo ya usafiri wa majini na usalama wa meli na
mazingira ya bahari.
Pia utafanya ukaguzi wa meli za kigeni na udhibiti wa meli
zilizosajiliwa nchini, udhibiti wa vivuko vya kibiashara, kudhibiti
shughuli za utafutaji na uokoaji, kudhibiti, kuratibu na kulinda
mazingira ya habari.
Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali, utahusisha Sheria ya
Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi Sura ya 216. Lengo ni kuondoa utata wa
vyombo vya utatuzi wa migogoro ya ardhi katika ngazi ya kata na wilaya
ambavyo vinatakiwa kuanzishwa katika mamlaka za wilaya pekee na si
mamlaka za miji.
Pia kutakuwa na marekebisho ya kuruhusu baraza la ardhi na nyumba la
wilaya kuwa na zaidi ya mwenyekiti mmoja na msajili wa baraza hilo kuwa
na sifa ya shahada ya sheria na uzoefu miaka 10.
Kwa mujibu wa muswada
huo, Sheria ya Upimaji wa Ardhi inayorekebishwa itawekwa kifungu kipya
kuruhusu kutambulika na kutumika kisheria kwa michoro yote ya upimaji na
ramani iliyotayarishwa kielektroniki.
Katika sheria ya mamlaka ya nchi kuhusu rasilimali za nchi ya mwaka
2017 kutaongezwa rasilimali za madini na mafuta. Pia kutafanyika
marekebisho ya sheria ya Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi sura ya 263
ambapo vipengele vinavyozungumzia malipo ya fidia kwa wafanyakazi
waliopata ulemavu wa kudumu wa chini ya asilimia 30 ya kila mwezi
yataondolewa na sasa malipo hayo ya fidia yatakuwa ya mkupuo.
Mbali na miswada hiyo, leo wabunge watapitisha Mapendekezo ya Mpango
wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali mwaka
2018/2019 ambao kwa wiki nzima iliyopita wabunge waliujadili na kutoa
mapendekezo yao.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 94 ya Kanuni ya Bunge Toleo la Januari 2016,
Bunge lilikaa kama kamati ya mipango ili kukidhi matakwa ya Ibara ya
639(3)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
kujadili na kuishauri Serikali kuhusu mapendekezo ya Mpango wa Taifa.
Sunday, November 12, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Geoffrey Mwambe, akiwaongoza wataalamu kutoka Wizara hiyo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi...
-
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy A. Mwalimu anapenda kutoa ufafanuzi kuhusu Tamko la Shiri...
-
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempongeza Mtendaji Mkuu wa timu ya Simba mwanadada Barbra Gonzalez kwa ubunifu na uzalendo wa hali ya juu kwa ...
-
Na Munir Shemweta, DODOMA Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ametangaza eneo lenye mgogoro wa muda mrefu la Mtakuj...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment