Mwamuziki wa muziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja ameibuka na
kusema kuwa, kabla ya kutokuwa maarufu alikuwa ni muhuni, mtukutu na
mwenye kiburi.
Dogo Janja amesema, kwa dunia hii ya sasa angekuwa jela au hata
marehemu kwani wenzake wengine wamepigwa mawe mpaka kufa kwa sababu ya
utukutu, unyang’anyi na matukio kama hayo.Aidha ameongeza kuwa, amejifunza kitu kutokana na makosa ndio maana ameamua kubadilika na kuachana na hizo tabia.
Mwanaspoti
Bongo Movies
0 comments:
Post a Comment