Afisa
manunuzi wa halmashauri Mr. Katunzi akikabidhi funguo za gari pamoja na
nyaraka za umiliki kwa Mkurugenzi Mtendaji ambapo naye atakabidhi kwa
Mwenyekiti wa Halmashauri.
Mkurugenzi Mtendaji Prof. Riziki Shemdoe,kulia katika picha ya
pamoja na Mwenyekiti wa Halamshauri Festo Mgina mara baada ya kupokea
nyaraka za umiliki wa Magari.
Halmashauri
ya Wilaya ya Mufindi imekamilisha mpango wake wa kununua Magari Mawili (2) mapya
kwa kutumia sehemu ya mapato yake ya ndani ya mwaka wa fedha 2016-2017 uliyokamilika
mwezi juni mwaka huu.
Taarifa
ya kitengo cha habari na Mawasiliano cha Halmashauri hiyo, imeyataja Magari
hayo kuwa ni Toyota Landcruiser Standard kwa gharama ya Sh. 187,680,373.11na Toyota
Hilux –Double Cabin kwa gharama ya Sh. 93,450,713, ambapo Magari yote mawili
yamegharimu Sh. 281,131,086.11.
Taarifa
hiyo imebainisha kuwa Magari hayo yamenunuliwa ili kukabiliana na changamo ya uchakavu
na upungufu mkubwa wa Magari uliyopo na kutanabaisha kuwa kati ya Magari hayo,
gari ya kwanza itatumiwa na Ofisi ya utala ambayo wakati wote hutakiwa kufika
kila kona ya eneo pana la Halmashauri lenye Majimbo mawili kata 27, Vijiji 121
na Vitongoji 562 kusimamia shughuli za maendeleo, huku gari ya pili ikinunuliwa
mahususi kwa shughuli za kukusanya Mapato.
Aidha,
Mchakato wa Manunuzi wa Magari hayo ambayo ni moja kati ya nyenzo muhimu za
kuharakisha maendeleo katika Halmashauri ya Mufindi, umefanyika kwa kufuata
taratibu zote za manunuzi ya Umma, ikiwa ni pamoja na kuomba kibali cha kufanya
manunuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakati mchakato mzima wa kuyanunua
ukitekelezwa na taasisi za zilizokasimiwa jukumu la manunuzi ya Umma, ambazo ni
TEMESA na GPSA.
0 comments:
Post a Comment