METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, November 3, 2017

MAVUNDE,LUSINDE NA KUNAMBI WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI NA KUELEZEA MIKAKATI YA DODOMA MPYA





Mbunge wa Jimbo la Mtera Mh.Livingstone Lusinde na Mbunge wa Dodoma Mjini  Anthony Mavunde wampongeza Mh. Rais Dk.John Pombe Joseph Magufuli kwa uamuzi wake kuhamishia Makao makuu ya Serikali Dodoma na hivyo kuongeza fursa za kiuchumi katika mkoa wa Dodoma kupitia uzalishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali zitakazotolewa.

Wakizungumza leo katika kipindi cha 360 cha Clouds TV wamesema uamuzi huo ni fursa muhimu kwa wanadodoma ni vyema wakaitumia ipasavyo.

Aidha  wamempongeza Mh. Rais Magufuli kwa uamuzi wake wa kuivunja CDA na kurudisha mamlaka ya utawala wa ardhi chini ya Manispaa ya Dodoma na kubadilisha mfumo wa umiliki ardhi kutoka katika upangaji(Lease Ground) kwenda kwenye mfumo wa hati ya umiliki.

Wamesema kupitia mfumo huo Dodoma itapata fursa ya kuvutia zaidi wawekezaji wa muda mrefu tofauti ilivyokuwa awali.

Aidha Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi ameelezea mipango mikubwa ya ukuzaji mji wa Dodoma ikiwemo uharakishwaji wa huduma ya vibali vya ujenzi,upimaji wa mae uboreshwa wa miundombinu na huduma za kijamii ili viende sambamba na ukuaji wa haraka wa mji wa Dodoma.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com